loader
Picha

ALIYEKUWA AKIIBIA FEDHA TRA KWA DAKIKA AZIREJESHA

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imewahukumu mfanyabiashara aliyetajwa na Rais John Magufuli kuiibia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mohamed Yusufali (39) Sh milioni saba kila dakika na wenzake kulipa faini ya Sh milioni 4.5 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukiri kuisababishia serikali hasara.

Pia mahakama hiyo imeamuru washitakiwa wote kulipa Sh 24,303,777,424.70 pamoja na kutaifisha nyumba nne zinazomilikiwa na Yusufali.

Washitakiwa wengine katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili ni Arifal Paliwalla (44) na Sameer Khan (40) ambaye ni Mfanyakazi wa Benki ya I & M.

Akitoa adhabu hiyo jana, Jaji Elinaza Luvanda alisema mshitakiwa Yusufali atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 3.5 au kifungo cha mwaka mmoja na miezi tisa na washitakiwa Paliwalla na Khan watatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja au kifungocha miezi mitatu gerezani.

Jaji Luvanda aliamuru mshitakiwa wa kwanza kulipa fidia TRA ya Sh bilioni 24.3 ambapo mpaka sasa ameshaingiza Sh bilioni moja na kumtaka kulipa fedha zilizobali kwa miezi 24 na kila mwezi atatakiwa kulipa Sh 970,990,726.8.

Pia alisema mali za mshitakiwa huyo zitataifishwa na kuwa mali ya serikali.

Alisema mshitakiwa wa tatu atatakiwa kulipa Sh milioni 10 kama fidia kwa hasara aliyosababisha TRA na tayari ameshaingiza kwenye akaunti Sh milioni moja na fedha zilizobaki atatakiwa kulipa ndani ya miezi 12 ambapo kila mwezi atatakiwa kulipa Sh 750,000.

“Mshitakiwa wa tatu anatakiwa kulipa fidia ya Sh milioni 300 na ameshalipa Sh milioni 200 bado Sh milioni 100 hivyo atatakiwa kulipa ndani ya miezi 10 na kila mwezi atalipa kwa usawa Sh milioni 10,” alisema Jaji Luvanda.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Pendo Makondo ameieleza mahakama kuwa washitakiwa wote ni wakosaji wa kwanza na hawana kumbukumbu ya makosa yao ya nyuma na kwamba wameingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Alidai Yusufali ameshaweka kwenye akaunti Sh bilioni moja kama fidia kwa TRA na kwamba kiasi kilichobaki ni zaidi ya Sh bilioni 23.3 hivyo, waliomba aendelee kulipa kwa miezi 24 na kwa kila mwezi anat- akiwa kulipa 970,990,726.8.

Pia aliomba mahakama hiyo itaifishe mali za mshitakiwa Yusufali ambazo ni maghorofa mawili yaliyopo Masaki,Dar es Salaam na mali zilizopo kwenye plot namba tatu na 46 huko wilayani Bagamoyo Pwani.

Kwa mshitakiwa wa pili, Makondo aliomba mahakama alipe fidia ya Sh milioni 10 na kwamba tayari ameweka kwenye akaunti Sh milioni moja.

Alidai mshitakiwa atatakiwa kulipa hasara hiyo kwa miezi 12 na kila mwezi atatakiwa kulipa Sh 750,000.

Mshitakiwa Khan ameshalipa Sh 200,000,000 kati ya 300,000,000 anazotakiwa kulipa fidia kwa TRA na fedha iliyobaki atatakiwa kulipa ndani ya miezi 10 na kila mwezi ni Sh milioni 10.

mawakili wa utetezi, wameiomba mahakama kuwapunguzia adhabu washitakiwa hao kwa sababu wamekiri na kujutia makosa yao hivyo, wameokoa muda wa mahakama na gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.

Pia waliomba majadiliano kati ya washitakiwa na DPP yanatakiwa kuendelea kwa sababu inamaliza kesi bila kupoteza muda.

Akisoma maelezo ya awali, Wakili wa Serikali Mkuu, Osward Tibabyekoma alidai washtakiwa walifanya udanganyifu kwa TRA kwa kuwasilisha nyaraka za uongo ili kuweza kupunguza malipo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyotakiwa kulipwa na kampuni Farm Plant.

Alidai ili kutekeleza vitendo hivyo katika tarehe tofauti kati ya Januari 2008 na Januari 2016 Yusufali alisajili kampuni mbalimbali kwa kutumia majina ya ndugu, marafiki na wafanyakazi bila wenyewe kuridhia au kujua.

Alidai alitumia usajili wa kampuni ili aweze kupewa hati ya usajili kama mlipa kodi na kupata mashine za kielektroniki (EFDs).

Kuendelea kudai kampuni zilizosajiliwa na mshitakiwa Yusufali hazikufanya kazi ya biashara kama alivyosajili na kwamba majina aliyoyasajili hayakuwa na uhusiano na kampuni lakini alilenga kuonesha yana uhusiano hivyo alitakiwa kulipa kodi kila mwezi.

Alidai mshitakiwa alionesha kampuni hizo zinafanya manunuzi zaidi ya kukuza hivyo kusababishia kulipa kodi kidogo. Tibabyekoma alidai washtakiwa kwa kuwasilisha nyaraka za uongo walisema kupunguziwa kodi wakati alitakiwa kulipa Sh bilioni 24.3.

Alidai mshitakiwa alifungua akaunti sita katika Benk ya I &M kwa majina ya ndugu na wafanyakazi wake ambayo ilikuwa ikitumika kuingiza fedha na pia alidai mshitakiwa Khan alimsaidia mshitakiwa Yusufali kufun- gua akaunti licha ya mapungufu ya wazi yaliyokuwepo kwenye nyaraka.

“Yusufali alikuwa na akaunti nyingine tano Equity benki ambayo zilitumika kufichua fedha zilizotokana na ukwepaji kodi.

Alisaidiwa na mshitakiwa wa pili kuhamisha fedha ambazo ni Dola za Marekani 1,550,000 kwenda kwenye akaunti tatu za Equity na akafanya manunuzi ya mali mbalimbali kwa kupitia kukwepa kodi,” alidai Tibabyenkoma.

Katika hatua nyingine, Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera amendika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ya kuomba kuanza majadiliano ya namna ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili.

Wakili wa utetezi, Jebra Kambole alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati jana hiyo ilipokuwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kuwa tayari wamepokea barua ya Kabendera na wanaishughulikia na itakapokamilika wataiarifu mahakama.

Hakimu Rwizile aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 24 mwaka huu.

Katika kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh milioni 173

Dodoma WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: Na Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

1 Comments

  • avatar
    Mima
    30/10/2019

    Nina Shaka hawa watu hawatalipa hizi fine. Ninanusa udanganyifu kwenye hukumu zinazotolewa. Billions 24.3 kulipwa kwa miezi 24 na ameishaweka bilioni moja tu, na billion 24 zilipwe within 24 months ama kifungo cha miezi 24, huu ni mchezo wa kuigiza. Huyu jamaa akishindwa kulipa billion 24, ambazobila Shaka wengi watashindwa, kukaa miezi 24 kwa bilioni 24 sio kazi kubwa. Rais Magufuli hizi hukumu zina Shaka ziangaliwe. Pesa zinazolipwa kwa watuhumiwa kuachiliwa ni kidogo sana zitapotelea njiani. Rais wangu najuwa unajitahidi lakini wezi bado wanatumia mbinu mpya.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi