loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga anzeni maandalizi mapema kuikabili Pyramids

WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa nchini, Yanga wiki hii waliwajua wapinzani wao watakaocheza nao katika mchezo wa Play-Off ili kupata nafasi ya kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wameangukia kwa Pyramids ya Misri, timu ambayo msimu uliopita ilimaliza katia nafasi ya tatu ya Ligi Kuu ya Misri na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi yao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Pyramids ni timu ya kawaida, licha ya kuwa na uwekezaji mkubwa kuliko vigogo wetu hapa nchini wa Yanga na Simba, hivyo wana wachezaji wazuri, ambao nao wamewasajili kwa fedha nyingi.

Yanga watacheza mchezo wa kwanza wa Play Off Oktoba 27 na wataanzia nchini kabla ya kurudiana Novemba 3 nchini Misri, ambapo mshindi wa jumla katika Yanga anzeni maandalizi mapema kuikabili Pyramids mechi hizo mbili, nyumbani na ugenini, ataingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Pamoja na uchanga wa Pyramids, ambayo imezidi- wa na Yanga kwa zaidi ya miaka 70, lakini hilo lisiwe tatizo la kuidharau timu hiyo, kwani ukubwa hauchezi mpira na pia ukubwa sio hoja.

Ni matumaini yangu kuwa Yanga Africans wataichukulia kwa makini sana ratiba hiyo na wakijiwekea malengo ya kufika mbali katika mashindano hayo na sio kuishia hatua hiyo ya makundi tu endapo watafuzu.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetenga kiasi cha kama dola za Marekani milioni 14 (ambazo ni zaidi ya sh bilioni 32), zitakazogawaywa kwa washindi wa hatua mbalimbali ya nane bora ya michuano hiyo.

Yanga sio tu wanagombea heshima katika soka hilo la Afrika, timu hiyo pia itapata fedha nyingi endapo itafanya vizuri katika michunao hiyo, kwani kila hatua kuna fedha zake.

Timu itakayokuwa bingwa wa mashindano hayo itaondoka na kitita cha dola za Marekani milioni 1.25 wakati mshindi wa pili dola Kinachotakiwa kufanya ni kujipanga vizuri kuanzia maandalizi kwa kucheza mechi za majaribio za kitafa na kimataifa ili kuendana na kazi ya wenzetu na ikiwezekana hata kucheza mechi za majaribio na timu za Misri milioni 0.626 huku timu zitakazoishia nusu fainali zipata dola za Marekani milioni 0.45 na wale wa robo fainali watapata milioni 0.35.

Yanga imeanza kushiriki kwa miaka mingi mashindano ya kimataifa kwa klabu, lakini haijawahi kufika mbali zaidi ya makundi, japo kufikia hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika au Kombe la Shirikisho.

Lakini msimu huu in- aweza kufanya kitu, endapo itaanza maandalizi yake mapema na kuondoa hofu ya kupangiwa kucheza na timu za Misri, ambazo zimekuwa zikitukanyaga kila kukicha.

Kinachotakiwa kufanya ni kujipanga vizuri kuanzia maandalizi kwa kucheza mechi za majaribio za kitafa na kimataifa ili kuendana na kazi ya wenzetu na ikiwezekana hata kucheza mechi za majaribio na timu za Misri.

Huu sio wakati wa maneno maneno, ila badala yake ni kujipanga vizuri ndani na nje ya uwanja kuhakikisha Pyramids hawatoki na wanapokea kichapo cha kutosha katika mchezo utakaofanyika jijini Dar es Salaam ili kurahisha kazi ugenini katika mchezo wa marudiano.

Yanga hakikisheni mnapambana kiume na kuipe- perusha vizuri bendera ya taifa letu, hasa mkijua kuwa nyinyi ndio wawakilishi pekee mliobaki katika michuano yote ya kimataifa.

UZURI wa ngozi huanzia ndani. Hivyo unavyoitunza ngozi yako kwa ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi