loader
Picha

Kigwangalla kuongoza Rock City Marathon

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla anatarajiwa kuongoza maelfu ya washiriki wa Rock City Marathon zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 20, kwenye viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall, jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Clement Mshana, ushiriki wa Waziri Kigwangalla unaenda sambamba na ushiriki wa viongozi wengine waandamizi wa serikali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ambaye tayari amethibitisha kushiriki.

“Uwepo wa Waziri mwenye dhamana na masuala ya utalii kwenye mbio hizi unatokana na yeye kuunga mkono agenda iliyobebwa na mbio hizi ambayo mbali na kukuza vipaji vya mchezo huo ni kutangaza utalii hususani katika ukanda wa Ziwa kupitia mchezo wa riadha,’’alisema.

Mbio hizo zilizo anzishwa miaka 10 iliyopita zinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili na maonesho ya waadau mbalimbali wa utalii.

Aidha, zikiwa zimesalia siku chache tu kabla ya kufanyika kwa mbio hizo, tayari wadau mbalimbali wanaotarajia kushiriki wameonesha kufurahishwa na zawadi zitakazotolewa kwa washindi na washiriki zikiwemo medali na fedha taslimu zaidi ya sh milioni 30.

“Pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh mil 2 kwa washindi wa pili na sh.

Milioni 1 kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi 15 watapata medali na fedha taslimu.

“Kwa upande wa mbio za kilomita 21, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia Sh milioni 2 kila mmoja, Sh milioni 1 kwa washindi wa pili na Sh laki 7 kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi na tano wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja,’’ aselima.

Kuhusu mbio za kilomita tano ambazo zitahusisha washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporates), Mshana alisema inatarajiwa kuwa zitaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi sambamba na washiriki wenye ualbino, ambapo zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi watatu wenye ualbino pekee.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi