loader
Picha

Aveva, Kaburu wamuangukia DPP

ALIYEKUWA Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu ‘Kaburu’ wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), wakiomba kuanza majadiliano ya namna ya kuimaliza kesi inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa kwa uamuzi kuhusiana na hoja mbalimbali zilizowasilishwa na upande wa mashitaka na utetezi.

Baada ya kuelezwa hayo, hakimu Simba alisema bado hajamaliza kuandaa uamuzi, hivyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 18, mwaka huu.

Ikumbukwe mahakama hiyo iliwaondolea mashitaka mawili ya utakatishaji, kati ya 10 yaliyokuwa yakiwakabili Aveva na Nyange Kaburu baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi yao.

Hata hivyo, washitakiwa hao pamoja na mwenzao Zacharias Hansppope walikutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka saba, ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa.

Kufuatia kuondolewa kwa mashitaka hayo ya utakatishaji washitakiwa wamepatiwa masharti ya dhamana kwa sababu mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliwanyima dhamana hayapo.

Kwa mujibu wa uamuzi huo uliotolewa na Hakimu Simba, ni jukumu la upande wa mashtaka kuthibitisha mashtaka yote kwa washitakiwa na kila shtaka linatakiwa kuthibitishwa peke yake na sio kwa kutegemeana.

 Baada ya kuchambua ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa mashitaka, ukiacha shtaka la tano na sita mahakama iliona kuwa washtakiwa wanakesi ya kujibu katika shtaka la 1,2,3,4,7,8 na 9 isipokuwa katika shtaka la tano na sita ambayo ni ya utakatishaji yaliyoondolewa.

Kufuatia kuondolewa kwa mashtaka hayo, Wakili wa washtakiwa hao Nehemia Nkoko aliiomba mahakama kuwapatia wateja wake dhamana kwani mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliyokuwa yanawanyima dhamana hayapo.

Wakili wa Takukuru, Leornad Swai alipoulizwa kama anapingamizi lolote juu ya dhamana alidai hawana pingamizi.

Hakimu Simba aliwapatia masharti ya dhamana washtakiwa ya kuwa na wadhamini waili watakaosaini bondi ya Sh milioni 30 kwa kila mmoja pamoja na kuwa na vitambulisho.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: Na Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi