loader
Picha

DED BARIADI MJI AVUNJA MKATABA UJENZI WA STANDI YA MKOA.

Halmashauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu imevunja mkataba wa ujenzi wa standi ya mabasi ya Halmashauri hiyo iliyokuwa inajengwa na wakandarasi wa ndani King's Buildersltd na Haleum Construction co.ltd kutokana na kusuasua kwa ujenzi huo.

Ujenzi huo wa standi ya Mkoa ulianza Novemba 2017 na kutakiwa kukamilika Novemba 2018 lakini mpaka sasa wakandarasi hao wako nje ya makubaliano ya mkataba huo na kusababisha ujenzi huo kusimama.

Akitoa tamko la kuvunjwa kwa mkataba huo leo mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Merckzedec Humbe amesema Halmashauri yake kupitia kamati ya fedha,baraza la madiwani na wataalam wake wameamua kuvunja mkataba huo na kutafuta mkandarasi mwingine atakayeweza kwenda na kasi inayotakiwa.

Amesema mbali na mkandarasi huo kuomba muda wa nyongeza na kuongezewa muda kwa vipindi viwili lakini kasi ya utendaji wake na utendaji wake umekuwa si mzuri.

"Hawa wakandarasi naona wametukwamisha sana, mbali na kuongezewa muda bado mradi huo unasua sua sana na tusipochukua hatua za haraka tutajikuta tunafikia muda wa ukomo wa mradi tumepangiwa na mfadhili mkuu ambae ni benki ya dunia" amesema Humbe

Mhandisi wa Halmashauri hiyo Mathias Mgorozi amesema kuwa mradi huo wa stand pamoja na barabara ya lami ya kilometa 1.5 kuzunguka standi hiyo unagharimu kiasi cha shilingi Bil 7.2 fedha za Mkopo kutoka benki ya dunia na Halmashauri inapaswa kuhakikisha inatumia fedha hizo kukamilisha jengo hilo kabla ya decemba 2019.

Nae mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amesema kamwe hatafumbia macho wakandarasi wazembe ndani ya Wilaya yeke na kuwa hawana nafasi kabisa.

Pia amemtaka mkurugenzi pamoja na mhandisi ujenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha ifikapo oktoba 15 ,mwaka huu mkandarasi mwingine aanze kazi Mara moja.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Na Happy Severine, Bariadi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi