loader
Picha

Ndege ATCL kukuza uchumi Katavi

RAIS John Magufuli amewataka wakazi wa Mkoa wa Katavi na mikoa jirani kutumia huduma ya usafiri wa ndege kujiimarisha kibiashara kwa kusafirisha mazao na kufanya shughuli nyingine za kibiashara.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa ndege wa Kampuni ya Ndege ya Serikali (ATCL) itakayokuwa ikienda Mpanda kila Jumatano ikitoka Dar es Salaam.

Rais alikuwa na ziara ya siku tisa katika mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi na ilimalizika jana.

Uzinduzi wa huduma ya ndege hiyo aina ya bombardier iliyoitwa jina la Mikumi, umetokana na agizo alilolitoa akiwa kwenye ziara yake mkoani humo la kuwa hatoondoka kurejea Dar es Salaam bila ya usafiri wa ndege hiyo.

Alisema kutokana na umuhimu wa huduma ya ndege kuelekea mkoani humo hakuona sababu ya kuchelewesha safari za kwenda mkoani humo na kusisitiza kuwa ana uhakika itakuza kilimo na utalii wa Katavi.

“Katavi ni mkoa wenye mambo mazuri mengi hasa kilimo, kwa kuwa huu ni mkoa wa nne kwa shughuli za kilimo nchini, una mazao mengi ambayo yote yanahitaji soko la uhakika… kuanzishwa kwa ndege hii kutawavutia wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza kwenye kilimo na shughuli nyingine na hivyo kuleta neema zaidi kwa wananchi, lakini pia utalii nao utakua kwa haraka zaidi hasa hifadhi ya Katavi hivyo ninawaomba msichoke kutambua na kuendeleza fursa zaidi zitokanazo na kilimo na utalii,” amesema

Rais Magufuli alisema serikali inakamilisha taratibu za ununuzi wa ndege nyingine kubwa mwaka huu itakayokuwa na uwezo wa kubeba watu 362 na pia imejipanga kuagiza ndege nyingine kubwa tatu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema kuwa ndege hiyo itakuwa ikitumia takribani saa moja na nusu kufika mkoani humo na kuwa itakuwa ikifanya kazi kila Jumatano.

Alisema lengo la muda mfupi ni kuhakikisha kuwa ndege hiyo inafanya kazi angalau mara tatu kwa wiki na lengo la muda mrefu iweze kufanya kazi kila siku na kuwataka wakazi wa Mkoa huo kuchangamkia huduma hiyo ya usafiri.

Kuachiwa kwa mafisadi

Rais Magufuli amebainisha kuwa hadi jana watu 135 waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi zikiwemo za utakatishaji fedha wameandika barua kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) na kuachiwa.

Amesema, kwa idadi hiyo inaashiria kuwa watuhumiwa hao wamemuelewa na kuwa wengine wataendelea kujitokeza na kuandika barua ya kukiri makosa yao na kuiomba ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kuwaachia.

Alimuagiza DPP kushughulikia nakala za maombi ya watu wengine zaidi ya 500 ambao nao wameonesha nia ya kuomba msamaha ili warejeshe fedha hizo zitakazotumika kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya nchi.

Kujiandikisha Daftari la Wapigakura Rais Magufuli pia ametishia kuwachukua hatua stahiki wakuu wa mikoa na wilaya ambao watashindwa kuhamaisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura.

Alisema ameshapata taarifa za mikoa na wilaya zinazoongoza hadi sasa kwa kujiandikisha kwenye daftari hilo huku akiitaka mikoa mingine ambayo haifanyi vema kujipanga na kuanza kufanya vema.

“Jamani msije kusema sikuwaambia mimi nitangojea tu ripoti ili mwisho wa siku kwa mikao na wilaya ambazo zitaonekana hazikufanya vema nitazichukulia hatua stahiki,”alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera alibainisha kuwa katika ziara hiyo Rais Magufuli ameidhinisha kiasi cha Sh bilioni 1.6 kwa ajili ya kuchenjua pamba na ni wazi kuwa uwekezaji zaidi utahitajika kwenye soko la pamba na kuwa ndege hiyo itawarahisishia wawekezaji wengi zaidi kufika Katavi.

Aliongeza kuwa licha ya kuanza kwa ujenzi wa bandari ya Kalema itakayofungua milango ya biashara kwa wafanyabiashara wa Katavi na Burundi lakini ndege hiyo itawavutia zaidi watalii huku akisisitiza uimarishwaji wa biashara ya samaki.

“Ujio wa Rais Magufuli mkoani kwetu umekuwa baraka kubwa kwa Mkoa huu kwa kuwa amerahisisha upatikanaji wa huduma ya usafiri wa ndege, ametupatia fedha za uchejuaji wa pamba na mengineo mengi, sisi tutatekeleza ushauri wake hasa katika kuendeleza sekta ya utalii, tutahakikisha kila mtu anaenda kutalii hasa katika vyanzo ambavyo vinapatikana kwetu hapa Katavi mojawapo ni mto mapacha ambao ukinywa maji yake unapata watoto mapacha,” alisema.

Baada ya kuzindua safari za ndege za ATCL, Rais Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth walisafiri kwa ndege ya ATCL aina ya Bombardier Dash 8 - Q400 kutoka Mpanda mkoani Katavi kwenda Dodoma alikokwenda kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura wa Serikali za Mitaa 2019.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi