loader
Picha

Barabara kuitangaza Kisarawe kimataifa

WADAU wa utalii wametabiri kuwa Wilaya ya Kisarawe itakua kimapato na kupata umaarufu kitaifa na kimataifa kutokana na utalii baada ya kufunguka kwa Barabara ya Dar es Salaam-Kisarawe hadi Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Julius Nyerere.

Chama cha Watembeza Watalii Kusini mwa Tanzania (STTGS) kupitia kwa katibu wake, Dioniz Kazungu kimesema vivutio vya utalii vilivyomo wilayani Kisarawe katika Mkoa wa Pwani vitafahamika na wakati huohuo safari za kwenda katika hifadhi hiyo zitakuwa nyingi ikizingatiwa wilaya ipo karibu na Jiji la Dar es Salaam.

“Kutoka Dar es Salaam hadi gati la kuingia hifadhi ya Mwalimu Nyerere kwa kupitia barabara hii, takribani Kilometa 180 ni saa nne. Hii ina maana sasa badala ya kufanya safari zile fupi za Mikumi, ambayo iko mbali, sasa safari nyingi zitakuwa kwa Mwalimu Nyerere National Park,” alisema Kazungu.

Alisema hayo hivi karibuni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kukutana na waongoza watalii na wadau wengine wa sekta ya utalii kwa lengo la kutangaza rasmi fursa zitokanazo na barabara hiyo.

Katika mkutano huo ambao waongoza watalii walifanya ziara kwenye vivutio mbalimbali vya utalii wakiongozwa na Ofisa Utalii wa wilaya, Kennedy Muhoza, Kazungu aliomba serikali kufanyia matengenezo sehemu korofi ambazo kipindi cha mvua hazipitiki.

Akipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuendeleza utalii Kusini na Magharibi ya Tanzania hususani kwenye hifadhi hiyo mpya ya Mwalimu Nyerere, Kazungu alisema “tunaomba ione umuhimu wa kutengenza kwa kiwango cha lami angalau mpaka gati la Mtemere ili kuongeza ufanisi wa kazi yetu.”

Kiongozi huyo wa waongoza watalii alisema hifadhi hiyo itakuwa ni ya kipekee na yenye mandhari nzuri ya kuvutia itakayoungana na hifadhi nyingine zilizotawanyika kikanda.

Alitaja kanda hizo na idadi idadi ya hifadhi kwenye mabano ni Kaskazini (tano), Magharibi (saba), Mashariki (tatu) na Kusini zipo tatu.

Akitaja fursa za uwekezaji katika utalii, Ofisa Utalii wa Wilaya, Muhoza, alisema Kisarawe ni wilaya  iliyo jirani na hifadhi ya Mwalimu Nyerere (kilometa 152).

Pia iko karibu na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na Jiji la kibiashara la Dar es Salaam kwa takribani kilometa 15.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi, Kisarawe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi