loader
Picha

Maji kupungua ifikapo 2025

MWENYEKITI wa Bodi ya Maji Taifa ya Wizara ya Maji, Profesa Hudson Nkotagu amesema ifikapo mwaka 2025 kila mtanzania anakadiriwa atapata wastani wa mita za ujazo wa maji 1,500 kiwango ambacho ni kidogo kimataifa.

Profesa Nkotagu ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Jiolojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLEO jijini Dar es Salaam.

Alisema upatikanaji wa maji kwa mwaka 2001 kila mtanzania alikuwa anapata mita za ujazo 2,007 kwa mwaka na hivi sasa anapata mita za ujazo 1,800 kwa mwaka. Alisema kimataifa mwanadamu yeyote anatakiwa asipate chini ya mita za ujazo 1,700 kwa mwaka.

“Tunashukuru Tanzania tupo juu ya kiwango cha kimataifa kwa sasa lakini ifikapo mwaka 2025 kila mtanzania anakadiriwa atapata wastani wa mita za ujazo 1,500 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi,”alisema.

Kwa upande mwingine alisema kuna kilomita za ujazo 96.27 za maji yanayofaa kunywewa kwa Tanzania kwa mwaka, lakini itakapofika mwaka 2035 kutakuwa na takribani mita za ujazo 833 kwa mwaka.

Alisema changamoto kubwa za upatikanaji wa maji inatokana na mabadiliko ya tabia nchi, uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji, ukuaji wa shughuli za kiuchumi na uongezekaji wa watu.

Awali alisema vyanzo vya maji nchini na duniani kote viko vya aina mbili ambayo ni maji yaliyoko juu ya uso wa dunia na yale yaliyoko chini ya ardhi.

Alisema maji yaliyoko juu ya ardhi yapo kwenye maziwa yakiwemo Victoria, Tanganyika, Rukwa, Nyasa na kwenye mabwawa kama Nyumba ya Mungu, kwenye mito midogo na mikubwa ikiwemo Ruvu, Wami, Pangani, Malagarasi, Ruvuma, Kagera.

“Hapa nchini chanzo ambacho kinatumika kutoa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ni vyanzo vyote vilivyoko juu ya ardhi hu- susan maeneo ya mjini,”alisema. Vijijini maji yaliyoko chini ya ardhi ndiyo hutumika kwa wingi.

Profesa Nkotagu alishauri kuongezwa kwa wataalamu wa kutosha katika sekta ya maji hususan wataalamu wa maji chini ya ardhi.

Pia alishauri serikali kuongeza uwekezaji katika kuperemba na kuchakata takwimu za rasilimali za maji nchi nzima chini na juu ya ardhi.

Ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika tafiti za vyanzo mbalimbali vya maji ikiwa ni pamoja na teknolojia ya kutibu maji taka kutoka kwenye majumba ya watu ili yaweze kutumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo ya nyumbani kama ya kunywa.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Na Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi