loader
Picha

Halmashauri yakwepa panga la Magufuli

HALMASHAURI ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa imejinasua mikononi mwa Rais John Magufuli baada ya kutangaza hadharani kuwa Ijumaa wiki hii itakuwa imehamia katika mji mdogo wa Laela, kuanza kazi rasmi ya kuwahudumia wananchi.

Katika zoezi hilo la kutoka katika Mji wa Sumbawanga na kuhamia rasmi katika mji mdogo wa Laela, halmashauri hiyo imepanga kutumia zaidi ya Sh milioni 55 kutoka katika makusanyo yake ya mapato ya ndani.

Akizungumza na gazeti hili, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Apolinary Macheta alisisitiza japo halmashauri hiyo ilikuwa imepewa siku 30 kuhakikisha inahamia rasmi katika mji mdogo wa Laela, imeweza kutekeleza agizo la RaisMagufuli ndani ya siku 14.

“Mchakato wa kupata ofisi tumeshaufanya tayari, pia namna ya kugawa majengo ya kufanyia kazi kwa kila idara...Ijumaa wiki hii ndio siku rasmi ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi wetu pale Laela kama halmashauri,”alibainisha.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Na Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi