loader
Picha

Mlemavu aliyejua kusoma nyumbani na kufunza wengine apewa baiskeli

MTOTO Sophia Hamis (10) ambaye ni mlemavu aliyejua kusoma na kuandika bila kuingia darasani juzi alipatiwa baiskeli yenye magurudumu maw- ili (wheelchair) itakayomwezesha kwenda shuleni.

Baiskeli hiyo alikabidhiwa mwishoni mwa wiki wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa iliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Membe kata ya Chilonwa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ndio ilitoa baiskeli hiyo kwa ajili ya kumrahisishia usafiri na kumwezesha kuweza kutimiza ndoto zake za kuweza kufika shuleni na kujifunza pamoja na wenzake.

Akikabidhi baiskeli hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga alisema hiyo ni faraja kubwa kwake kwani Sophia kutokana na ulemavu wake hakuweza kuandikishwa shuleni lakini anajua kusoma na kuandika na anafundisha watoto wengine.

Pia mtoto huyo alikabid- hiwa cheti cha kuzaliwa ambacho pamoja na mambo mengine kitamuwezesha kupata Toto Afya Bima itakayomsaidia kupata matibabu aliyoyakatiza ya viungo na baadae kutimiza ndoto yake ya kutembea.

Baba mzazi wa Sophia, Hamisi Yona alishukuru serikali kwa msaada huo utakaowezesha binti yake kufika shuleni.

Alisema binti huyo ni mlemavu wa miguu lakini anaweza hata kutambaa hali ambayo inamtia moyo kuona kuwa anaweza kuanza masomo.

Alisema serikali iendelee kumsaidia mtoto huyo pamoja na kumpatia matibabu yatakayo- saidia kuimarisha afya yake.Yona alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa mlemavu.

Alisema hakukuwa na njia nyingine ya kumsaidia Sophia zaidi ya kubaki nae nyumbani hali alipoibuliwa na walimu wa shule ya msingi Membe na hatimaye taarifa zake kuandikwa magazetini na hatimaye kupatiwa msaada wa baiskeli.

Katika shule ya msingi Membe tayari wametengeneza miundombinu itakayowezesha baiskeli anayotumia Sophia kupanda ili kufika darasani.

Hata hivyo Ofisa maendeleo ya Jamii katika wilaya ya Chamwino, Sophia Swai alisema changamoto iliyopo sasa ni namna ya binti huyo akifika shuleni atawezeje kujisaidia kwani amekuwa akitambaa na vyoo vilivyopo havina miundombinu ya watu wenye ulemavu.

“Hili la choo ndio tunalianga- lia sasa kama kitachimbwa choo kwa ajili yake au kutafutwa shule yenye miundombinu rafiki ili aanze kusoma.

Kwa upande wake mtoto huyo alisema anashukuru kwa msaada huo.

Pia mtoto huyo alikabidhiwa nguo na viatu vilivyotolewa na wadau mbalimbali.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Na Sifa Lubasi, Chamwino

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi