loader
Picha

Stars yaivaa Amavubi leo

TIMU ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo jioni itakuwa na kibarua kigumu ugenini kuwakabili wenyeji Rwanda ‘Amavubi’, kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika katika Uwanja wa Nyamirambo, jijini Kigali, Rwanda.

Mchezo huo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa), Stars watautumia kupata matokeo chanya ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kupanda kwenye viwango vya mchezo huo duniani.

Aidha, kwenye mchezo huo, Stars wanahitaji ush- indi kuchagiza maandalizi ya mchezo ujao wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) kwa kucheza na Sudan Oktoba 18 nchini Uganda.

Katika mchezo huo dhidi ya Sudan, Stars wanahitaji zaidi ushindi wa angalau mabao 2-0 ili kutinga fainali hizo za Chan zitakazofanyika Cameroon 2020 baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha msaidizi wa Taifa Stars, Sulemani Matola, jana alisema wachezaji wote wanaunda kikosi hicho wako fiti na wanachosubiri ni wakati ufike waweze kuingia uwanjani kwa kusaka ushindi.

Alisema maandalizi ya kikosi hicho yamejikita kupata ushindi ili kuwa- tengenezea wachezaji hao wazingira ya kujipanga na mchezo ujao wa marudiano dhidi ya Sudan, ambao wana amini utakuwa mgumu kwakuwa watakuwa ugenini.

“Wachezaji wote wapo tayari kwa maana ya kuwa fiti kwa mchezo huo na kila mmoja anajua tunajukumu zito la kupata matokeo, kwanza tupande kwenye viwango vya Fifa, lakini pia tunahitaji ushindi ambao utazidi kuwapa nguvu wachezaji dhidi ya Sudan,” alisema Matola.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: Na Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi