loader
Picha

NYOTA SIMBA WAMKUNA AUSSEMS

KOCHA wa timu ya Simba, Patrick Aussems, amefurahishwa na ki- wango kilichooneshwa na wachezaji wake kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Bandari kutoka Kenya.

Amesema mchezo huo umem- saidia kubaini makosa yaliyopo katika kikosi chake hicho, ambacho hadi sasa kinaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo, Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alisema mchezo huo ulikuwa maalumu kwa kuwapima wachezaji wake na kuweka miili yao sawa katika kipindi hiki ambacho ligi hiyo imesimama kupitisha kalenda ya Fifa kwa Stars kucheza dhidi ya Rwanda leo.

Aidha, Aussems alisema mchezo huo ulimpa nafasi kama mkuu wa benchi la ufundi kuwapima wachezaji wake wengine ambao hawajumuishwi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo kuonesha uwezo wao.

“Nimefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wangu mbele ya Bandari ambao nao wamecheza kwa umakini mkubwa wakihitaji ushindi na mazoezi ya leo ni mazuri kwa wachezaji wangu kujipanga na mechi za ligi,” alisema Aussems.

Alisema baada ya mchezo huo timu hiyo inatarajia kuanza safari ya kwenda Kigoma kucheza mechi mbili za kirafiki na moja ya kimataifa, michezo yote inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: Na Tuzo Mapunda

1 Comments

  • avatar
    Shukuru
    15/10/2019

    Michezo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi