loader
Picha

Mtaka ampinga Simbu mgogoro RT

RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka amesema kuwa hakuna mgogoro wowote unaoendelea kati yao.

Mtaka ameyasema hayo jana mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea kauli ya mwanariadha nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu kukutofanya vizuri katika mashindano ya 17 ya riadha ya Dunia kulisababishwa na kutoandaliwa vizuri kutokana na mgogoro uliopo ndani ya RT.

Simbu alisema hivi karibuni kuwa timu ya Tanzania iliyoshiriki mashindano hayo Doha, Qatar haikupata maandalizi yoyote kwa sababu viongozi wa RT walikuwa wakiendeleza malumbano tu na kumsusia jukumu hilo Katibu Mkuu wake, Wilhelm Gidabuday.

Hata hivyo, Mtaka alikiri kutokuwa na maandalizi mazuri kwa timu ya Tanzania iliyoshiriki mashindano hayo kama walivyo- fanya kwa mashindano yaliyopita ya dunia jijini London 2017 na Olimpiki Brazil 2016.

Alisema Simbu alikuwa na haki ya kuliongelea hilo kutokana na maandalizi yalitopita viongozi, makocha na wachezaji wote kuwa kitu kimoja, lakini sasa walijiweka kando baada ya RT kuandaa kambi Eldoret, Kenya, lakini wanariadha walikataa wakisisitiza kufanya mazoezi Arusha chini ya makocha wao.

Alisema pamoja na kuandaa kambi, lakini katika utekelezaji pamoja na Simbu mwenyewe walidai Arusha watafanya vizuri zaidi, jambo ambalo lilipigwa na uongozi pamoja na yeye (Mtaka), kwani alijua wazi hakutakuwa na medali kwa maandalizi ya Arusha.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: Na Cosmas Mlekani

1 Comments

  • avatar
    Christopher
    15/10/2019

    Mtusaidie kutumia vizuri maneno ya Kiswahili hasa kwa ajili ya vijana wetu wanao chipukia sasa katika lugha, mfano kwenye gazeti la leo mmeandika 'Mtaka asema Simbu ajitambui' kiswahili sahihi ni ajitambui au hajitambui?

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi