loader
Picha

Harambee Stars hoi kwa Msumbiji

FRANCIS Kimanzi amepata pigo la kwanza kama kocha wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, baada ya timu yake kufungwa na Msumbiji katika mchezo wa kimataifa wa kirafi ki juzi.

Bao la kipindi cha pili lililofungwa na Canhembe Amancio lilitosha kuwawezesha wageni kupata ushindi wao wa kwanza katika majaribio manne katika mchezo huo dhidi ya Harambee Stars na kuwanyima Wakenya nafasi ya kutamba nyumbani.

Kipigo hicho kimekuja siku moja baada ya mwanariadha wa Kenya wa marathon, Eliud Kipchoge kuweka historia katika mbio hizo Vienna, Australia Jumamosi. Kipchoge amekuwa binadamu wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili baada ya kutumia saa 1: 59:40 wakati wa mbio hizo zilizojulikana kama INEOS 1:59 nchini Australia.

Kipchoge, ambaye alikuwa akisaidiwa na wanariadha 41, ameingia katika kitabu cha kumbukumbu cha Guinness kwa kukimbia marathon chini ya saa mbili. Jumapili, Wakenya walisheherekea mafanikio mengine baada ya Brigid Kosgei kuvunja rekodi ya dunia kwa wanawake kwa zaidi ya dakika moja katika Chicago marathon.

Kosgei alitimua mbio kirahisi na kuweka rekodi hiyo ya dunia kwa kutumia saa 2:14: 04, akipunguza dakika moja na sekunde 21 kutoka ile ya awali iliyokuwa ikishikiliwa na Muingereza Paula Radcliff aliyoiweka mwaka 2003.

Kwingineko, Kenya imefuzu kwa mara ya pili mfululizo kucheza Michezo ya Olimpiki licha ya kufungwa katika fainali katika mashindano ya wanawake ya rugby ya Afrika yaliyofanyika huko Monastir.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi