loader
Picha

Taifa Queens bado hakijaeleweka

TIMU ya taifa ya netiboli ya Tanzania, Taifa Queens, leo inatarajia kuanza mazoezi rasmi kujiandaa na mashindano ya Afrika yatakayofanyika Pretoria, Afrika Kusini kuanzia kesho, Oktoba 16 hadi 23, imeelezwa.

Kocha wa timu hiyo, Argentina Daud alithibitisha jana kuwa leo anatarajia kukutana kwa mara ya kwanza na wachezaji wa timu hiyo, ambayo inatarajia kupiga kambi ya kudumu katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Mgulani jijini Dar es Salaam. Daud alisema kuwa leo baada ya kukutana na wachezaji wanaounda timu hiyo pamoja na viongozi wa Chaneta, ndio atakuwa na la kuzungumza zaidi uhakika wa timu hiyo kuondoka lini na kama itaenda katika safari hiyo na mambo mengine.

“Kesho (leo) baada ya kukutana na wachezaji na viongozi wa Chaneta (Chama cha Netiboli Tanzania) na ndio nitakuwa na taarifa rasmi za maandalizi ya timu na kama tunakwenda Afrika Kusini na mambo mengine, “alisema Daud kwa njia ya simu jana.

Alipoulizwa kama timu hiyo imeshawi kufanya mazoezi, Daud alisema kuwa hawajawahi ila leo ndio atakutana na wachezaji kwa mara ya kwanza na kuzungumza nao. Awali akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa Chaneta, Dk Marwa alisema kuwa timu hiyo leo itaanza kambi ya kudumu kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuondoka kwenda Afrika Kusini.

“Wachezaji leo wataanza kambi ya kudumu pale katika kambi ya JKT Mgulani kwa ajili ya mashindano hayo ya Afrika, “alisema Marwa.

Alisema serikali imewaahidi tiketi na kuwataka kuandaa kila kitu, tayari kwa safari hiyo ya Afrika Kusini, ambapo timu hiyoina inatarajia kwenda na wachezaji 12, viongozi watatu.

Tanzania katika mashindano hayo ya Afrika imepangwa katika Kundi A pamoja na wenyeji Afrika Kusini, Malawi na Zambia huku Kundi B likijumuisha timu za Uganda, Zimbabwe, Kenya na Eswatini.

Endapo Taifa Queens itashiriki, basi yatakuwa mashindano yao ya kwanza tangu Tanzania ifunguliwe na Shirikisho la mchezo huo la kimataifa (INF) baada ya ‘kutengwa’ kutokana na malimbizo ya muda mrefu ya ada.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi