loader
Picha

Kocha Rayon matumain kibao

KOCHA wa Rayon Sports Janvier Martinez Espinosa amewataka wachezaji wake kusahau matokeo yaliyopita dhidi ya Gasogi United na kufanya kweli katika mchezo wa leo wa uzinduzi wa Ligi Kuu ya Ewanda.

Rayon Sports Jumamosi ililazimishwa suluhu dhidi ya Gasogi United na hivyo inataka matokeo katia mchezo wa leo. Mabingwa hao watacheza dhidi ya AS Kigali ambayo iliwafunga hivi karibuni katia mchezo wa Super Cup, ukiwa ni uzinduzi wa Ligi Kuu, ambao watafungua nao dimba dhidi ya mabingwa wa Kombe la Amani.

Espinosa anahitaji ushindi dhidi ya AS Kigali lro katika mchezo wa pili wa ligi ini kukwepa kuwa katika presha kubwa na mashabiki wa timu hiyo inayojulikana kama the Bues.

“Ingawala tulilazimishwa suluhu na Gasogi, kuna kitu cha kufanya ili kuhakikisha tunashinda mchezo huo. Mchezo dhidi ya AS Kigali utakuwa mgumu lakini nina imani na timu yangum itashinda mchezo huo, “alisema Espinosa.

AS Kigali, ambayo ni miongoni mwa timu inayopewa nafasi kubwa ya kushinda ligi msimu huu, iliwabana APR kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa Jumamozi.

Kwingineko, Bugesera itakuwa mwenyeji wa APR katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Nyamata. Bugesera ilianza vizuri msimu mpya wa ligi ikiifunga Heroes FC 2-0. Mabao yote nawili yamlifungwa na Jimmy Mbaraga.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi