loader
Picha

Nyota Arsenal kuwashawishi wenzake kutembelea Rwanda

NYOTA wa klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya England, David Luiz anasema kuwa alikuwa na kipindi kizuri sana wakati alipoitembelea Rwanda na kuahidi kuwa atawashauri marafi ki zake kutembelea nchi hiyo.

“Nimefurahia kila kitu nchini Rwanda tangu siku yangu ya kwanza, na ninategemea kurudi tena siku za baadae.”

Beki huyo Mbrazil aliyasema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati akikamilisha ziara yake hiyo ya siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa Kigali Convention Centre Jumamosi jioni.

Miongoni mwa maeneo mengine aliyoyatembelea Luiz ni pamoja na eneo la kumbukumbui ya mauaji ya kimbali, ambako alitoa pole kwa waathirika wa mwaka 1994 kabla hajatembelea Mbunga ya taifa ya Volcanoes, Pia alipokewa na Rais Paul Kagame katika kijiji cha Urugwiro. Ziara ya mchezaji huyo ilikuwa ni sehemu ya mpango wa miaka mitatu wa ‘Zuru Rwanda’ kati ya Serikali ya Rwanda na klabu hiyo ya Uingereza, ambao ulianza rasmi Mei 2018.

“Nilipata nafasi ya kukutana na sokwe wa ajabu na pia nilitembelea sehemu nyingine kibao. Nitakwenda kuwashawishi marafiki zangu Brazil na Ulaya kutumia likizo zao nchini Rwanda, “alisema Luiz ambaye alijiunga Arsenal akitokea kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu Chelsea Agosti.

Kama sehemu ya mpango huo wa Kutembelea Rwanda, wachezaji kutoka timu ya wanawake na wanaume za Arsenal zimekuwa zikitembelea Rwanda huku makocha wakiendesha kambi ya mafunzo ili kuendeleza mchezo wa soka nchini humo kwa wavulana na wasichana.

“Wengine atakaotembelea Rwanda ni wachezaji watatu wa timu ya kwanza ya wanawake ya Arsenal. Ni jambo zuri kwa Rwanda kuwawezesha wanawake, “alisema Peter Silverstone, Mkurugenzi wa Fedha wa Arsenal.

Bila kutaja tarehe halisi, Kageruka alisema majina ya wachezaji hao watatu yatatangazwa baadae.

QUIQUE Setien anasema kuwa hawezi kufi kiria jinsi alivyokuwa akiota ...

foto
Mwandishi: KIGALI, Rwanda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi