loader
Picha

NEMC yaonya wauza maji kweye vifuko vya plastiki

BARAZA la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewatahadharisha na kuwaonya wauzaji rejareja wa maji na bidhaa nyingine wanaotumia mifuko laini ya plastiki kwamba wanavunja sheria, kwani mifuko hiyo pia imepigwa marufuku.

Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka alisema mifuko hiyo japo imepigwa marufuku, kasi ya kuitumia inaongezeka na wachuuzi wanaitumia kuuza maji na kufungia bidhaa nyingine ndogondogo.

Alisema maji yanayouzwa kwenye mifuko hiyo hayana usalama pia kwa matumizi ya binadamu kwa sababu hayajathibitishwa ubora. Katika Jiji la Dar es Salaam, mifuko hiyo laini inatumika kuchuuza rejareja maji yanayoitwa ‘kandoro’ na bidhaa nyingine kama vile karanga, bisi na kadhalika. Kiongozi huyo alisema kurudi kwa maji hayo mitaani kunatishia usalama wa afya za watu na mazingira. “Licha ya kwamba hiyo mifuko hairuhusiwi, hatujui maji hayo yanatoka wapi.

Hali hii inahatarisha afya ya mlaji. Kama kweli ni mjasiriamali na unataka kuzalisha na kuuza maji basi nenda TBS na hivyo vifungashio na maji yako, wakapime waangalie maji unazalishia eneo gani. Ukifika pale watakuratibu.

“Kwa sasa maji hayo hayaruhusiwi kabisa,” Dk Gwamaka amewaeleza waandishi ambao wanaofuatilia utekelezaji wa marufuku ya serikali juu ya matumizi ya mifuko ya plastiki.

Dk Gwamaka alisema taasisi yake ina jukumu la kuunga mkono sera za serikali juu ya bishara, viwanda na kuboresha maisha ya wananchi na kwa hiyo inaunga mkono wajasiriamali wabunifu na wawekezaji. Lakini aliongeza kwamba jukumu la pili muhimu ni kuhakikisha sheria zinafuatwa ili kulinda afya ya wananchi na mazingira.

“Msimamo wetu juu ya mambo haya tunaueleza wazi kabisa,” aliwaambia waandishi hao. Alisema timu ya watumishi wa NEMC ipo mtaani kwa ajili ya ukaguzi wa mazingira hivyo atakayekutwa akitumia mifuko hiyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kifungo au faini kutokana na vifungu vya sheria za kutunza mazingira.

“Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, alikwishaeleza kwamba hayo maji hayaruhusiwi. Niwaombe Watanzania kutoa ushirikiano katika kutunza mazingira yetu kwa kutoa taarifa pale ambapo kuna uvunjifu wa sheria ya mazingira. Piga simu namba 0800110116 au andika ujumbe kwenda namba 0683540344. Simu yetu haina gharama,” alieleza.

Dk Gwamaka aliwaonya wanaozalisha na kusambaza wa mifuko mbadala ambayo haikidhi vigezo vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwamba watachukuliwa hatua. Alitaja baadhi ya vigezo kwamba ni pamoja na kuwa na uzito usiopungua 70GSM, anuani ya mzalishaji au nembo ya biashara na kuthibitishwa na TBS.

Alisema si lengo la baraza hilo kukwamisha biashara bali usalama wa binadamu na mazingira yake ni moja ya vipaumbele vyake. “Ni muhimu kwetu kumtambua mmiliki wa mifuko hiyo ili ikitokea tatizo kwenye suala la viwango tujue wakushughulika naye...,” Hatuwezi kukiuka viwango vilivyowekwa na ndiyo maana kuna baadhi ya mifuko imezuiliwa bandarini hadi leo kwasababu taratibu na sheria zilizowekwa hazijafuatwa,” alisisitiza Dk Gwamaka. Mkurugenzi wa Sheria wa NEMC, Bernard Kongoza alisema baraza linafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi kuhakikisha sheria za mazingira zinafuatwa.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi