loader
Picha

Bandari Kisumu kuchochea uchumi Afrika Mashariki

UKARABATI mkubwa uliofanywa katika Bandari ya Kisumu nchini Kenya umeifanya bandari hiyo ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini humo kuwa kichocheo cha uchumi wa taifa hilo na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Wananchi wa Kenya wana hamu kubwa kuona bandari hiyo ikizinduliwa rasmi katika kiwango cha hali ya juu tofauti na ilivyokuwa awali ambapo utendaji wake ulikuwa usio wa viwango.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, wakuu wa nchi zote sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanatarajiwa kuhudhuria siku ya uzinduzi wa bandari hiyo unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Bandari ya Kisumu imefanyiwa ukarabati mkubwa kwa gharama ya Sh bilioni tatu za Kenya, ingawa kuna mipango ya kuifanyia marekebisho makubwa zaidi ambapo Sh bilioni 22.5 zitatumika.

Rais Uhuru Kenyatta pamoja na mjumbe wa Umoja wa Afrika (AU) katika Maendeleo ya Miundombinu, Raila Odinga, wataongoza uzinduzi wa mradi huo unaotajwa kuwa wa kihistoria kutokana na kwamba utanufaisha mataifa yote ya Afrika Mashariki kwa wakati mmoja.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: KISUMU

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi