loader
Picha

JPM alivyoonesha njia kubadilisha maisha Kusini

IPO wazi kuwa juhudi ya serikali kwa sasa ni kuhamasisha uanzishaji wa viwanda ili kufi kia uchumi wa viwanda ifi kapo 2025. Safari ya kuelekea uchumi wa viwanda haiwezi kutekelezwa pasipo kuhusisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi kwani asilimia 70 ya Watanzania ni katika kilimo.

Msimu wa mavuno ya korosho wa mwaka 2018/2019 umekuwa fundisho na ufunguo wa fursa nyingi zilizojificha na sasa zinakwenda kwa kasi. Katika kuhimili misukosuko ya soko, aliyekuwa Waziri wa Kilimo wa wakati huo, Dk Charles Tizeba alikutana na wabanguaji wadogo wa korosho ili kubaini changamoto na namna ya kuzipatia ufumbuzi ili ubanguaji usonge mbele.

Hata baada ya Rais John Magufuli kuagiza korosho zinunuliwe na serikali, hatua mbalimbali zilichukuliwa ikiwamo kutambua viwanda mfu na hai vya kubangua korosho ili kuona namna vinavyoweza kusaidia. mikoa ya Mtwara na Lindi walifuata nyayo za Rais kwa kutembelea viwanda vya korosho walikobaini uchakavu wa mashine na kutafuta njia bora zaidi za kufufua viwanda hivyo.

Kwa kuangalia msimu uliopita na wakati msimu mwingine wa korosho umeingia, Rais John Magufuli bado anajua mahitaji halisi ya wakulima wa korosho, mahitaji ya ubanguaji wa korosho zao. Ndiyo maana katika hafla ya kupokea magari 40 kutoka Serikali ya China, Rais Magufuli anasema anahitaji msaada wa kujengwa kwa kiwanda kikubwa cha kubangua korosho mkoani Lindi.

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli anasema japo China miradi 723, anapenda mradi wa 724 uwe mradi unaohusu kiwanda kikubwa cha korosho kitakachosimamiwa majeshi ya nchi hizi mbili. Ukiangalia mapambano anayoendesha Rais Magufuli kufanikisha kuinua maisha ya wakulima wa korosho, utabaini wazi kuwa, inabidi watendaji wa mikoa inayolima korosho wachukue hatua kuelekea Lindi au Mtwara ya viwanda.

Watanzania wote wanapaswa kujua kuwa, ni jukumu lao kujiletea maendeleo na kwamba, ni hatari kusubiri mtu mwingine atusaidie na tukiwa watu wa namna hii tutachelewa kufika tunakokwenda kimaendeleo.

Tunatakiwa tujipange na kujituma wenyewe kwa kuchukua hatua za kwanza kutumia tulicho nacho ili misaada itukute njiani. Hatuna budi kujiunga katika vikundi na kupata mafunzo mbalimbali hasa kutoka Shirika la maendeleo ya Viwanda vidogo (Sido) na kisha, tuanze kubangua korosho na tujitafutie mauzo kwa kuimarisha masoko ya ndani.

Katikati ya vijiji vya Mkwaya na Njonjo kipo kikundi maarufu cha ubanguaji korosho ambacho ni mfano na bora wa kuwa na vikundi vingi vya namna hii ili korosho zetu zibanguliwe kuwa tayari kwa soko la ndani na nje. Kwa kuendeleza teknolojia ndogo za machine za ufugaji, ubanguaji, usindikaji wa bidhaa katika taswira ya viwanda vidogo vidogo huku tukisubiri hisani kutoka kwa wenzetu wa nje.

Nimeanza kuzungumzia korosho Kusini kwa kuwa ndiko Rais Magufuli alipoanza kuonesha njia ya watu wa Kusini kupita, lakini kama tunataka kubadilisha maisha, siyo tu tunatakiwa kuangalia njia hiyo, bali pia kuifuata bila shuruti tukielewa tulipotoka, tulipo na tunapokwenda. Fikiria wakulima wa minazi, miembe, ufuta, mihogo na alizeti wa mikoa ya Pwani Kusini ikiwamo Lindi na Mtwara ina minazi ya kutosha.

Hata hivyo, swali katika mikoa yetu ya Lindi na Mtwara ni kuwa, vikundi vingapi vimejiunga na kutumia minazi na bidhaa zake kujinufaisha kupitia viwanda vidogo? Tuzingatie kuwa, katika nazi tunaweza kutengeneza vyakula kama kashata au kutengeneza tui la nazi, kutengeneza sabuni nakadhalika. Kutokana na maganda ya nazi, tunaweza kupata usumba unaotengeneza zulia.

MTWARA ni mkoa unaojivunia kuwa na maliasili nyingi na maeneo ...

foto
Mwandishi: Abdulrasul Elhaji

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi