loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Magufuli amaliza mgogoro wa Lindi Vijijini

MVUTANO uliodumu kwa muda mrefu kuhusu wapi kujengwe Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini, umemalizwa na Rais John Magufuli jana.

Rais Magufuli ametamka rasmi kuwa Makao Makuu ya halmashauri hiyo yatakuwa Mtama na itaitwa Halmashauri ya Mtama na siyo Lindi Vijijini. Aidha, amerejea kauli ya kumsamehe Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (CCM) kutokana na madhambi aliyomtenda ya kumsema vibaya baada ya sauti yake kuvuja mitandaoni.

Rais Magufuli ameanza ziara ya kikazi mkoani Lindi ambayo jana alipokuwa akienda wilayani Ruangwa alilazimika kusimama kwenye baadhi ya vijiji kikiwemo Kiwalala, Mtama, Nanganga na vinginevyo na kuongea na wananchii waliojitokeza barabarani.

Aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuendelea kumuunga mkono mbunge wao Nape kwa kuwa alishamsamehe kwa dhambi zake alizotenda na kuwaahidi wananchi wa jimbo hilo ambao hawajalipwa fedha zao za korosho kuwa mpaka ifikapo siku ya Jumanne wiki ijayo watakuwa wamelipwa.

Akiwa kijijini Kiwalala, Rais Magufuli alisikitishwa na mvutano uliokuwepo kuhusu wapi kujengwe Makao Makuu ya halmashauri hiyo huku baadhi wakitaka yajengwe Sudi wakati wengine wakitaka yajengwe ama Mchinga au Londo, hali iliyomfanya mkurugenzi na watendaji wake kuweka ofisi zao katika Manispaa ya Mkoa wa Lindi.

Kutokana na mvutano huo, Rais Magufuli alitamka Makao Makuu hayo yawe Mtama na kufuta jina la Halmashauri ya Lindi Vijijini na badala yake akaagiza iitwe Halmashauri ya Mtama na kumtaka waziri mwenye dhamana kulisimamia jambo hilo ili liwepo kisheria. Katika hilo pia alizitaka Halmashauri za Bunda mkoani Mara na Korogwe mkoani Tanga zenye mgogoro kama huo wa Lindi Vijijini kuhakikisha wanapata ufumbuzi ndani ya siku 15.

Kuhusu wakulima wa korosho wa Lindi Vijijini ambao hawajalipwa fedha zao, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alimweleza Rais kuwa mpaka ifikapo Jumanne ijayo, jumla ya Sh milioni 43 zitalipwa kwa wakulima hao kwa kuwa uhakiki wa akaunti zao umeshakamilika.

Kauli hiyo ya Bashe ilikuja baada ya Nape kumweleza Rais kuwa wakulima wote wa korosho katika jimbo lake walishalipwa fedha zao isipokuwa wakulima 24 tu.

Pamoja na Nape kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia Sh bilioni 1.5 kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya, Rais aliwaeleza wananchi hao kuwa kuna upotevu wa Sh milioni 86 katika ujenzi wa Hospitali ya Mkoa ya Sokoine, lakini pia gari aina ya Toyota Land- Cruiser kuuzwa kinyemela, hivyo aliagiza fedha na gari hilo virudishwe haraka.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi