loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majaliwa aita wakurugenzi Dar sakata la skimu ya maji Lindi

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda ya Kusini, wafi ke ofi sini kwake Dar es Salaam leo asubuhi wakiwa na taarifa kuhusu Skimu ya Umwagiliaji ya Narunyu mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vyombo vya habari, Majaliwa aliagiza hivyo jana mchana wakati alipokwenda kukagua skimu hiyo iliyokuwa ikilalamikiwa tangu mwaka2017. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama ni Warioba Gunze na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda ya Kusini ni Mhandisi Mndeme.

Alichukua uamuzi huo baada ya kufika kwenye eneo la mradi na kupokea malalamiko ya wanajumuiya ya umwagiliaji kutoka kwa Mwenyekiti wao, Bakari Awadhi juu ya kusuasua kwa mradi huo, lakini alipotaka kupewa maelezo na wataalamu, hakuwepo hata mmoja ili kutoa maelezo. “Nilitarajia niwakute hapa Mkurugenzi wa Halmashauri, Ofisa Umwagiliaji wa Wilaya na Mkurugenzi wa Umwagiliaji wa Kanda. Nimeagiza wanikute Uwanja wa Ndege Lindi au Dar es Salaam na kesho asubuhi waje ofisini kwangu wanipe taarifa kamili ya mradi huu. Nataka nijue fedha zilizobaki, zaidi ya Sh mil 240 ziko wapi,” alisema Waziri Mkuu.

Majaliwa alisema alitoa taarifa kuhusu ujio wake kwenye eneo hilo hivyo walipaswa kuwepo. Alisema amepata taarifa kuwa wamesafiri nje ya Mtwara na kwamba asubuhi ya leo walikuwepo Lindi Mjini.

“Waje ofisini kesho (leo), wakishindwa nitachukua uamuzi mwingine,” alisema.

Akielezea umuhimu wa mradi huo wakati akizungumza na baadhi ya wanaushirika waliokuwepo, Waziri Mkuu alisema ni wa muhimu kwa sababu unatiririsha maji wakati wote.

Alisema ni mradi wa kuringia kwakuwa unatiririsha maji mengi hata wakati wa kiangazi. Alisema kutokana na umuhimu wa mradi huo, wangekuwa wanazalisha mazao ya kila aina.

“Hapa ni mahali pa kuzalisha mazao mengi, leo unalima mahindi, ukivuna unapanda matikiti, ukitoa unapanda nyanya. Sasa nitapasimamia mwenyewe,” alisisitiza.

Aliwataka wanaushirika wanaounda jumuiya hiyo ya umwagiliaji wahakikishe kila mmoja anatambua eneo lake na mara kazi ikianza wawe tayari kuanza kilimo. Alisema mradi huo una manufaa kwa watu wa Ruo, Mahumbika hadi Mnazi Mmoja na kwamba ni lazima ung’ang’aniwe kwa sababu kuna idadi kubwa ya wakulima wanaoutegemea. Waziri Mkuu alipofika Uwanja wa Ndege wa Lindi, maofisa hao walikuwa hawajafika na simu zao hazikupatikana.

WILAYA tatu za mkoa wa Lindi za Nachingwea, Ruangwa na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi