loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mahiga: DPP bado ameweka kifuani taarifa za wahujumu

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Balozi Augustine Mahiga amesema Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga bado ameweka kifuani taarifa za watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliopewa nyongeza ya siku saba na Rais John Magufuli ya kuandika barua za kuomba msamaha.

Septemba 30, mwaka huu baada ya DPP kutoa taarifa yake kwa Rais Magufuli Ikulu, Dar es Salaam baada ya kukamilisha kazi ya kupokea barua za watuhumiwa wa kesi za uhujumu uchumi walizokiri makosa yao, kuomba msamaha na kukubali kurejesha fedha za serikali, alimwomba Rais amwongezee siku tatu kwa sababu kulikuwa na baadhi ya watuhumiwa walikosa nafasi ya kuandika barua hizo.

Sababu zingine alizitoa Mganga za kuongezewa muda ilikuwa ni changamoto alizokumbana nazo ikiwamo barua kuandikwa kwa mkono na baadhi ya washitakiwa walikuwa wakihudhuria kesi zao mahakamani, hivyo hawakupata nafasi ya kuandika barua hizo, ndipo Rais aliongeza siku saba badala ya siku tatu alizoombwa.

Kwa kuwa siku saba za nyongeza zilikwisha tangu wiki iliyopita, gazeti hili lilitaka kujua kutoka kwa Waziri Mahiga kama kulikuwa na mtuhumiwa yeyote aliyejitokeza kutumia nyongeza hiyo ya siku saba za Rais na ndipo aliposema DPP Mganga ameweka taarifa za jambo hilo kifuani mwake.

WATOTO 84,625 waliokuwa na utapiamlo mkali, wametibiwa kuanzia mwanzoni mwa ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi