loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ndalichako amkalia kooni Kamishna wa Elimu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amempa siku 14 Kamishna wa Elimu na wataalamu wake kumpa mrejesho wa maagizo aliyotoa Julai mwaka huu, kuhusu kurekebisha Waraka wa Elimu unaompa nafasi mwanafunzi kuomba ruhusa ya kutohudhuria masomo kwa siku 90, ili kuzuia utoro kwao.

Profesa Ndalichako alisema hayo katika mahafali ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Bogwe wilayani Kasulu mkoani Kigoma, akieleza kuwa Waraka wa Elimu kumpa siku 90 mwanafunzi kutoonekana shule bila kuhudhuria shuleni, ndiyo chanzo kikubwa cha utoro mkubwa kwa wanafunzi nchini.

“Nimempa maagizo Kamishna wa Elimu nchini akae na wataalamu wake waufanyie mapitio waraka huo na kuurekebisha, maagizo nimempa tangu Julai hadi leo sijapata mrejesho wowote. Na sasa nampa siku 14 kuhakikisha kazi hiyo imefanyika na kinyume chake kamishna atafute maelezo ya kuridhisha kwa nini nisimuadhibu,” alisema.

Alisema wakati waraka unatoa siku 90 kwa wanafunzi, inashangaza kuona waalimu wanapewa siku tano wasipoonekana shule wanakuwa wamejifukuzisha kazi.

Alisema jambo hilo si sawa kwani halina uwiano kiuhalisia. Aidha, aliwataka wanafunzi nchini na hasa wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kufanya mitihani hivi karibuni kujibidiisha kwenye masomo ili wafaulu.

Alisema serikali inatumia fedha nyingi kwenye uwekezaji wa elimu na kwa sasa kupitia Mpango wa Lipa kwa Matokeo (EP4R), hadi Septemba mwaka huu serikali imetumia Sh bilioni 308 kutekeleza mpango huo. Katika hilo, alisema jumla ya madarasa 2,898 yamejengwa, mabweni 535, nyumbani za walimu 66, matundu 6,629 ya vyoo huku shule kongwe za sekondari 62 kati ya 88 kwa thamani ya zaidi ya Sh bilioni 300 zimekarabatiwa.

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ameagiza mbegu bora za ...

foto
Mwandishi: Fadhil Abdalla, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi