loader
Picha

Wahusika kashfa makontena 38 kuchukuliwa hatua

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene ametangaza kuwa serikali itawachukulia hatua wote waliohusika na kashfa ya makontena 38 ya chuma chakavu yaliyokuwa yasafi rishwe kwenda nje, lakini yakazuiliwa bandarini Dar es Salaam.

Katika ripoti ya uchunguzi iliyowasilishwa kwake juzi, imeeleza kuwepo kwa udanganyifu mkubwa wa kusafirisha bidhaa ambazo hazimo katika orodha ya vitu vilivyoruhusiwa kusafirishwa nje kama chuma chakavu au taka hatarishi.

Akipokea taarifa hiyo, Simbachawene alisema uchunguzi umeibua mambo mengi na kwamba serikali itawachukulia hatua kali wahusika wote katika kashfa hiyo.

“Ripoti inaonesha kumekuwa na hujuma kubwa ya miundombinu ya nchi; kwa mfano mifuniko ya chemba za maji, nyaya za umeme na mataruma ya reli, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na tarabitu za biashara ya chuma chakavu,” alieleza na kuongeza “Ripoti imebaini kuwepo kwa kampuni isiyo na kibali cha kufanya biashara hiyo”.

Alisema kampuni hiyo (hakuitaja) itafutiwa leseni ya biashara na nyingine zitakazoonekana zimefanya udanganyifu na kuhujumu uchumi nazo zitawajibishwa.

Simbachawene alifanya ziara Bandarini Dar es Salaam, Agosti 9, mwaka huu. Baada ya kuyaona makontena 38 ya chuma chakavu yaliyozuiliwa bandarini, alilagiza Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamzi wa Mazingira (NEMC) kuwasilisha serikalini taarifa juu ya makontena hayo.

“Nimeliagiiza baraza kuyafanyia kazi mapendekezo yote ya ripoti hii ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wafanyabiashara wote waliohusika na makontena hayo,” alieleza.

Alisema serikali imekuwa ikiingia hasara kubwa kutokana na udanganyifu wa wafanyabiashara kwa kusafirisha bidhaa zisizo katika orodha ya vyuma chakavu. Alieleza kuwa katazo la serikali la kusafirishwa vyuma chakavu na taka hatarishi nje ya nchi limetokana na udanganyifu wa wafanyabiashara.

“Katazo hilo lengo lake ni kulinda viwanda vyetu vinavyotegemea vyuma chakavu kama malighafi ya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo nyaya za umeme na mikeka ya plastiki,” alieleza.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi