loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbowe, wenzake watakiwa kujitetea kwanza

UPANDE wa mashitaka katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam itoe mwongozo utakaowataka washitakiwa hao kutoa utetezi wao kabla ya mashahidi.

Hayo yamebainishwa jana na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kuwasilisha hoja nne za kupinga utaratibu wa kusikiliza mashahidi kabla ya washitakiwa hao uliotolewa na upande wa utetezi.

Nchimbi alidai ombi la upande wa utetezi la kuanza kusikiliza mashahidi kabla ya washitakiwa wenyewe kutoa utetezi, halitekelezeki kwa sababu linakiuka sheria ya ushahidi na mwenendo wa mashauri ya jinai inayotoa mwongozo wa kuendesha na kusikiliza mashauri.

Alidai kifungu cha 144 cha Sheria ya Ushahidi sura 6 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 kinazungumzia uongozaji wa mashahidi. Alidai wanashawishi mahakama kwamba utaratibu wa uwasilishaji mashahidi wakati wa utetezi unatamkwa na kifungu cha 231 (1) (a) na (b) pamoja na mambo mengine kinazungumzia haki na utaratibu wa kuwasilisha utetezi.

“Mshitakiwa hawezi kuingia kwenye haki ya kuita mashahidi kama yeye mwenyewe hajaamua au hajatoa ushahidi. Mahakama ijielekeze pia katika kifungu cha 38 (2) (a) na (b) kwani utaratibu wa utoaji wa ushahidi wa utetezi mahakama inapaswa kumwita mshitakiwa kama ushahidi ili atoe utetezi wake,” alidai Nchimbi.

Alidai washitakiwa wanavaa kofia mbili kwa wakati mmoja kwa sababu wanasimama kama washitakiwa na mashahidi kwa wakati mmoja.

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na vyombo ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

1 Comments

  • avatar
    Medy Mgeleka
    18/10/2019

    Comment Asa Mbn Iy Kesi Inayumb

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi