loader
Picha

Waziri ataka Tanesco kutoa taarifa wanaosambaziwa umeme

NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi wa usambazaji wa umeme vijijini kwa viongozi wa vijiji na wananchi wa maeneo husika ili wafahamu hatua zaidi za utekelezaji wa miradi hiyo.

Mgalu alisema hayo kwa nyakati tofauti juzi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuzindua na kuwasha umeme katika Kijiji cha Mpiji, Kata Boko katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani na kukagua maendeleo ya Mradi wa Usambazaji Umeme vijiji vya Kiluvya, Misugusugu, Mkombozi na Mtaa wa Mwambisi wilayani humo.

Naibu Waziri alisema Tanesco wakiweka utaratibu wa kuzungumza na viongozi wa vijiji pamoja na wananchi mara kwa mara juu ya hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi husika, kutaondoa maswali mengi pamoja na wasiwasi walionao wananchi dhidi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa usambazaji wa umeme.

“Unajua Watanzania ni waelewa sana, unapompa mtu taarifa ya kile kinachofanyika katika eneo lake kwa wakati sahihi inamfanya awe na amani na waliopewa dhamana,” alisema Mgalu.

Aliwaeleza Watanzania ambao hawajafikiwa na miradi ya usambazaji wa umeme kuwa na subira wakati serikali inaendelea kutekeleza kazi hiyo kwa awamu, kwa kuwa si jambo jepesi kuwafikia wananchi wote kwa siku moja.

Alisema lengo la serikali ni kufikisha huduma ya umeme kwa kila Mtanzania, na kueleza kuwa serikali ilipoingia madarakani vijiji 2018 tu, ndiyo vilikuwa na umeme, sasa hivi idadi imeongezeka na kufikia zaidi ya vijiji 8,100 na tayari zaidi ya vijiji 6,000 vimeunganishwa, lengo ni kuvifikia vijiji vyote 12,319 nchi nzima ikifikapo Juni 2021.

Katika mazungumzo yake na wakazi wa Kijiji cha Misugusugu, aliitaka Tanesco kuwafungia wateja, transfoma inayokidhi mahitaji ya umeme katika kijiji hicho na maeneo yanayowazunguka ili kuondoa adha ya kukatika umeme katika eneo hilo mara kwa mara ambayo inasababishwa na kulemewa kwa transfoma iliyopo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Kibaha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi