loader
Picha

Bosi TPSF mbaroni upotevu wa mabilioni

MWENYEKITI wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte na viongozi wa kampuni ya Katani Limited, wametiwa mbaroni na Polisi mkoani Tanga, wakihusishwa na upotevu wa zaidi ya Sh bilioni 54, zikiwemo za serikali.

Shamte ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Biashara kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na wenzake walikamatwa jana kulitokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Edward Bukombe na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Christopher Mariba.

Shigella alitoa agizo hilo baada ya kupokea ripoti ya Mkaguzi wa Ndani wa Hesabu za Serikali aliyoitoa katika mkutano wa wadau wa mkonge, iliyoonesha kuwa kampuni hiyo ina upotevu wa zaidi ya Sh bilioni 54. Waliokamatwa kwenye mkutano huo mbali na Shamte ni Mkurugenzi Mtendaji wa Katani Limited, Juma Shamte, Fadhil Mhina ambaye ni Mhasibu wa Katani Limited, Mkurugenzi Fatma Diwani na Ofisa Mahusiano, Theodora Mtegeti.

Awali, akiwasilisha ripoti ya ukaguzi huo, Mkaguzi wa Ndani Mwandamizi- Wizara ya Fedha na Mipango, Idrisa Ally, alieleza kuwa ukaguzi huo ulianza Januari 22 hadi Februari 22, mwaka huu, ukijumuisha mwaka 2008 hadi 2018. Ally alisema ukaguzi huo ulilenga kuangalia miamala ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSSF), wakulima na fedha za Saccos ya wakulima hao, na mikataba mbalimbali iliyoingiwa baina ya pande zote tatu.

Alisema katika ukaguzi huo, zaidi ya Sh bilioni 54 hazikufahamika zilipo au matumizi yake hayakujulikana vyema; miongoni mwa hayo ni madeni ya wakulima, makato ya wanachama wa NSSF, mikopo na kutolipwa kwa kodi ya serikali kwa mujibu wa taratibu.

Alisema yaliyojitokeza katika ukaguzi huo ni madeni ya wakulima ya Sh bilioni 29.8 ambazo hazijaoneshwa kwenye taarifa za kampuni hiyo, Sh bilioni 1.7 za makato waliyokatwa wakulima huku Saccos ya wakulima ikiidai kampuni hiyo Sh milioni 5.55.

Hata hivyo, ripoti ya mkaguzi huyo ilionesha fedha zinazodaiwa na kampuni hiyo kwa wakulima kuwa ni zaidi ya Sh bilioni 2.8. Baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa kwenye mkutano huo na Mkuu wa Mkoa kutoa nafasi kwa pande zote kujieleza, mmiliki wa Katani Limited, Salum Shamte alisimama na kukanusha ripoti iliyowasilishwa akidai haina usahihi na hawakushirikishwa katika kuiandaa.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Korogwe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi