loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru yaokoa mil 800/- za makusanyo

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rukwa (Takukuru) mkoani Rukwa imeokoa zaidi ya Sh milioni 800 zikiwa ni fedha za makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri zilizokusanywa na wakusanya ushuru kati ya Mei Mosi na Oktoba mwaka huu.

Wakusanya ushuru hao, maofisa watendaji wa kata na vijiji wanatuhumiwa kuzitumia baada ya kukusanya zaidi ya Sh bilioni moja na kutoziwasilisha akaunti za halmashauri zao. Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Rukwa, Hamza Mwenda alibanisha hayo wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika jana mjini hapa.

Tukio la hivi karibuni limetokea ndani ya wiki mbili ambapo maofisa hao wamerejesha Sh 113,339,459 walizozikusanya lakini zilikuwa hazionekani kwenye akaunti za halmashauri zao. Limetokea baada ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo kuwakabidhi watumishi umma 42 wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Kalambo na Nkasi kwa Takukuru mkoani Rukwa kwa uchunguzi wa upotevu wa Sh bilioni moja.

Sh bilioni moja hizo ni makusanyo ya mapato ya ndani katika halmashauri hizo tatu naWangabo alitoa siku saba zirejeshwe. Wangabo alifikia uamuzi huo katika kikao maalumu cha wakurugenzi, waweka hazina, wahasibu na watendaji wa vijiji na kata wa halmashauri zote nne mkoani hapa ambao mfumo wa ukusanyaji mapato halmashauri (LGRCIS) unaonesha fedha za makusanyo hayo ya mapato ya ndani uko mifukoni mwao.

Katika kikao hicho, kila mkusanya ushuru alipewa nafasi ya kueleza sababu ya kutowasilisha makusanyo hayo ya ndani katika mfumo au benki ambapo baadhi yao walidai walipewa vibali na wakurugenzi wa halmashauri kuzitumia kabla ya kuziingiza katika mfumo na wengine hawakuwa na sababu za msingi.

“Baada ya Mkuu wa Mkoa (Wangabo) kutukabidhi watuhumiwa hao ndani ya wiki mbili, Sh 113,339,459 zimerejeshwa ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Sh 81,650,000 zimerejeshwa huku Sh 83,000,000 zipo katika utaratibu wa kulipwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuwa alitoa kibali cha fedha hizo kutumika nje ya mfumo,”alieleza.

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Sh 21,174,800 zimerejeshwa huku watumishi 13 wanachunguzwa kwa kutumia Sh 21,174,800 kinyume na utaratibu.

“Katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi zimerejeshwa Sh 92,000,000 huku Sh 55,000,000 bado hakijarejeshwa kutokana na baadhi ya watoza ushuru kutoroka na wengine kufunguliwa kesi mahakamani kutokana na kutafuna fedha walizozikusanya” alibainisha Mwenda.

Aliongeza kuwa licha ya watoza ushuru hao kurejesha fedha hizo bado Takukuru itawasiliana na mamlaka ya nidhimu aliwaadhibiwe kwa kukiuka taratibu na maelekezo ya Tamisemi

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na vyombo ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi