loader
Picha

Sekta ya viwanda kuajiri asilimia 40 ya vijana 2025

NAIBU Waziri, Ofi si ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amewataka vijana kuondokana na dhana ya kukimbilia ajira za ofi sini, badala yake wajiajiri na kujihusisha na biashara.

Pia amesema serikali inatarajia ifikapo mwaka 2025, asilimia 40 ya nguvu kazi ya nchi ambayo ni vijana itakuwa imeajiriwa katika sekta ya viwanda. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika hafla iliyowakutanisha vijana zaidi ya 100 waliochanguliwa kujiunga na programu ya ‘Vijana 2jiajiri’ inayoratibiwa na Benki ya KCB, waziri huyo alisema serikali inatengeneza mazingira wezeshi kwa vijana yatakayowasaidia kujiajiri na wengine kuajiriwa.

Alibainisha kuwa ukuaji wa viwanda nchini ndio nyenzo kubwa itakayofanikisha jambo hilo. Alisema pamoja na serikali kutengeneza mazingira hayo, vijana wanapaswa kuondokana na dhana ya kufikiria kwamba ili waonekane wana ajira ni lazima wafanye kazi maofisini, badala yake wahakikishe wanajiajiri.

“Tatizo vijana wengi wana fikra mbaya ya kuajiriwa na wanawaza kuwa lazima wavae shati jeupe asubuhi, suruali nyeusi na kwenda ofisini, mimi nawaomba wabadilike na waondokane na fikra hiyo kuanzia sasa, mnapaswa kujiajiri, kwa kufanya shughuli yeyote inayowaingizia kipato,”alisema.

Tafiti za mwaka 2014 zinaonesha nchi ina uwezo wa watu milioni 24.3 wa kufanya kazi, hivyo watu hao kila mwaka wanaingia katika soko la ajira. Naye, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam, Violet Fumbo alisema programu ya ‘Vijana 2jiajiri’ inayosimamiwa na Benki ya KCB ni mkombozi kwa vijana wengi kwani itawasaidia kupata elimu ya ufundi stadi itakayowawezesha kufanyakazi za ujasiriamali.

Alisema kijana yeyote atakayepata fursa ya kupata elimu ya ufundi na ujasiriamali anapaswa kuondokana na dhana ya kuajiriwa na kuongeza kuwa VETA ipo tayari kushirikiana na KCB ili kuwasaidia vijana kutimiza malengo yao. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB, Cosmas Kimario alisema jumla ya Sh milioni 80 wamezitoa ili kuwasaidia vijana 123 kupata elimu ya ufundi stadi katika chuo cha VETA na baadaye kujiajiri.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi