loader
Picha

Takukuru yaonya wagombea serikali mitaa kuhusu rushwa

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Tanga (Takukuru) imetoa onyo kwa wagombea uongozi katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani ambao watajitoa dakika za mwisho.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Christopher Mariba alitangaza kiama kwa wagombea hao wakati akitoa taarifa ya taasisi hiyo ya mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu kwa Mkoa wa Tanga alipozungumza na waandishi wa habari hapa. Mariba alielezea mikakati ya taasisi hiyo kuelekea uchaguzi zijazo itafanyia kazi mambo ambayo chaguzi za awali zilizopita yalikuwa yakifanywa kiholela na kinyume cha sheria.

Kwenye chaguzi za serikali za mitaa Novemba 24 mwaka huu na mwaka 2020 hatutakuwa na mgombea atakayejitoa dakika za mwisho na atakayefanya hivyo hatua kali zitachukuliwa kwake.

Kuhusu miradi, Mariba alisema miradi 33 ya maendeleo yenye thamani ya sh 7842,182,458.76 sekta ya elimu inayotekelezwa mkoani Tanga na kubaini baadhi yake ina dosari mbalimbali. Miongoni mwa dosari ambazo Takukuru imezibaini ni udokozi mkubwa wa fedha za ruzuku zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kupeleka kwenye shule za Halmashauri za Mkoa wa Tanga.

Alisema katika ufuatiliaji huo,Takukuru imebaini kuwepo kwa ukiukwaji taratibu za manunuzi kwa baadhi ya miradi ya ukarabati majengo ya Serikali hasa shule na ununuzi wa vifaa kwa matumizi ya shule na maeneo mengine hakuna uwazi.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Tanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi