loader
Picha

Ni Stars na Sudan leo

TIMU ya Taifa ya Soka ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kushuka dimbani leo ugenini kuikabili Sudan katika mchezo wa kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan 2020).

Mchezo huo utachezwa ugenini kuanzia saa 1:00 usiku, huku Stars ikiwa imetoka kupoteza mchezo wa kwanza bao 1-0 uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ni mchezo muhimu kwa Taifa Stars kuhakikisha inapata matokeo ya ushindi kuanzia mabao 2-0 na kuendelea ili kupata nafasi ya kufuzu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10 Tanzania ilipofuzu kwa mara ya kwanza mashindano hayo yalipofanyikia Ivort Coast.

Timu hizo zina historia mara ya kwanza katika michuano kama hiyo ya kufuzu zilikutana Dar es Salaam na Stars kushinda 3-1 kisha ziliporudiana Stars ikashinda tena 2-1 ugenini. Lolote linawezekana kama tu Stars itakuwa imejipanga vizuri dhidi ya mpinzani wake huyo. Beki wa Stars, Erasto Nyoni alisema maandalizi yako vizuri na anaamini watapata matokeo mazuri.

“Sisi tuko salama hakuna mtu mwenye majeruhi na tumejiandaa vizuri, kikubwa ni Watanzania kutuombea heri tupate matokeo mazuri,”alisema.

Stars kabla ya kuvaana na Sudan ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Rwanda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo ambapo licha ya kutoka suluhu Kaimu Kocha Mkuu Ettiene Ndayiragije aliwatumia wachezaji wengi wa ndani kuwapa mazoezi.

Katika michezo iliyopita safu ya ushambuliaji ilionekana kuwa butu kwa kutengeneza nafasi nyingi na kushindwa kufunga, lakini ameongezwa mshambuliaji mpya Ditram Nchimbi hivyo, huenda mambo yakawa mazuri. Sudan imekuwa ikicheza mchezo wa kujilinda na mashambulizi ya kushtukiza na ilifanya hivyo katika mchezo wa kwanza labda watacheza kwa kufunguka zaidi leo. Timu hizi zimekutana baada ya Stars awali kuwatoa Kenya.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi