loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga kuiua Pyramids inawezekana, lakini...

IMEBAKI wiki moja na siku kabla ya wawakilishi pekee wa Tanzania hawajashuka kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kucheza dhidi ya Pyramids ya Misri katika mchezo wa mchujo kwa ajili ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo muhimu utapigwa Jumapili ya Oktoba 27 kwenye uwanja huo, kabla timu hizo hazijarudiana na mshindi wa jumla wa mechi hizo mbili, atakata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga, inahitaji kuweka rekodi ya kuziondoa timu za Waarabu, kwani wawakilishi wetu hao hawana historia nzuri kwa kuwa wamekuwa wakitolewa na timu za ukanda huo wa Afrika Kaskazini.

Pamoja na Yanga kutokuwa na rekodi ya kuwaondoa Waarabu katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, lakini timu hiyo inaweza kama tu itafanya maandalizi yake vizuri ndani na nje ya uwanja.

Hilo linawezekana. Pyramids ni timu changa ambayo haina uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa ukilinganisha na Yanga, ambao wameshiriki kwa miaka mingi.

Yanga katika wiki hii iliyobaki, wanatakiwa kuwa makini na maandalizi na itakuwa vizuri zaidi kama timu itaweka kambi Mwanza ili kuzoea hali ya hewa na hata Uwanja wa CCM Kirumba.

Bila shaka Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera atakuwa ameshaisoma Pyramids na kujua nguvu za udhaifu wake uko sehemu gani na kuutafutia dawa ya kuwafunga mabao mengi ili kujiweka katika nafasi nzuri tukielekea mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 3 Misri.

Hakuna lisilowezekama katika soka, kwani kikubwa ni maandalizi ya uhakika ndani na nje ya uwanja ili kuhakikisha washambuliaji wa Yanga wanakuwa makini wanapolikaribia lango la wapinzani huku mabeki kutofanya makosa ya mara kwa mara, kwani Waarabu ni wazuri kutumia makosa ya wapinzani.

Nje ya uwanja, mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha Uwanja wa CCM Kirumba unajaa na kufurika na wakati wote mashabiki wanatakiwa kuwashangilia wawakilishi wetu bila kuchoka, kuhakikisha Mwarabu hatoki.

Yanga imewahi kuifunga USM Alger 2-1 na kutoka sare na Al Ahly na Mo Bejaia lakini iilishindwa kupata ushindi wa jumla na kujikuta ikitolewa katika katika awali au kushindwa kufanya vizuri katika makundi.

Ni matarajio yetu Yanga itawafunga Pyramids, lakini kinachotakiwa ni kuongeza umakini na kuibuka na mabao mengi katika mchezo huo wa kwanza ili kuhakikisha wanapata ushindi wa jumla baada ya mchezo wa pili.

RIPOTI ya 15 kuhusu uchumi wa Tanzania ya ...

foto
Mwandishi: Tahariri,

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi