loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Man City yafanya mauaji Etihad

MABINGWA wa Ligi Kuu ya England, Manchester City jana walifanya kweli baada ya kuibuka na mzito wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad.

Ushindi huo umepunguza tofauti ya pointi kati yake na vinara wa ligi hiyo kwa sasa, Liverpool ambao leo watashuka dimbani kucheza dhidi ya Tottenham katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.

Man City pamoja na ushindi huo mnono, lakini walikuwa na kazi kubwa ya kufanya katika kipindi cha kwanza, ambapo hadi kinamalizika, timu hizo zilikuwa suluhu.

Mabao ya wash indi katika mchezo huo yalifungwa na R Sterling (46), K De Bruyne (65), I Gündogan (70) na Fernandinho ( 87). Raheem Sterling alifunga bao lake la sita katika mechi nne kwa klabu hiyo.

Man City sasa itakuwa mwenyeji wa Southampton in katika mchezo wa raundi ya nne ya Kombe la Carabao raundi ya 16 katika mchezo utakaofanyika Jumanne kabla ya Jumamosi ijayo haijacheza dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

MOHAMED Salah, alifunga mara mbili na kusaidia mabingwa Liverpool kufi ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi