loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Meneja mwendeshaji benki ya Exim afungwa maisha

MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Arusha imemfunga kifungo cha maisha jela Meneja Mwendeshaji wa Benki ya Exim Tawi la Arusha, Livingstone Mwakihaba (37) maarufu kwa jina la Stone kwa kosa la kughushi nyaraka ya benki na kumwiba mteja wa benki hiyo kiasi cha Sh milioni 565.

Hukumu hiyo iliyoandikwa na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Obadia Bwegoge kabla ya kuhamishwa kikazi na kusomwa na Hakimu Mfawidhi, Rose Ngoka ilisomwa Ijumaa wiki iliyopita katika mahakama hiyo, ilidaiwa kuwa Stone alitenda kosa hilo mwaka 2012 akiwa meneja kabla ya kufukuzwa kazi.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa dakika 25, Stone alikutwa na kosa hilo baada ya kubainika kuwa Novemba 28, 2012 akiwa Meneja Mwendeshaji wa benki hiyo alighushi karatasi ya malipo ya benki ya amana ya kudumu yenye kumbukumbu namba EB/97/011148 ikionesha kuwa mteja Daniel Urio (56) alimweka kiasi cha Sh milioni 565 katika benki hiyo wakati sio kweli kwani fedha hizo ziliingia mfukoni mwake..

Hukumu hiyo ilisema kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ilionesha wazi kuwa mteja aliweka kiasi hicho cha fedha kwa kufuata taratibu zote za kuweka ikiwamo kujaza fomu na kupewa fomu aliyojaza akiamini fedha zake ziko mahali salama kumbe sio kweli kwani alipewa fomu bandia iliyoghushiwa na Stone.

Iliongeza kuwa kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, fomu hiyo na mtaalamu wa maandishi, iligundulika kuwa Stone alighushi nyaraka za benki na kusaini kumlaghai mteja Urio fedha Sh milioni 565 pamoja ziliingia benki wakati fedha hizo ziliingia mfukoni mwa Stone wakati akijuwa wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Hukumu iliongeza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu Kifungu 338, kitendo cha kughushi nyaraka ya benki na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kifungo chake ni kwenda jela maisha hivyo mahakama hiyo inamfunga Stone kifungo cha maisha ili iwe fundisho kwa wafanyakazi wengine wa benki wenye tabia kama hiyo isiyokuwa ya uaminifu kwa wateja na kuichafuliwa jina benki.

“Kwa hiyo mahakama inakutia hatiani kwa kosa hilo kwa kwenda jela kifungo cha maisha ili iwe fundisho kwa wafanyakazi wengine wa benki wenye tabia hiyo kuwaibia wateja wa benki na kuchafua jina la benki,” ilisema.

Mahakama ilimwachia huru mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo, Urio ambaye ni mfanyabiashara wa madini ya tanzanite mjini Mirerani baada ya mashahidi wote katika kesi hiyo kushindwa kuthibitisha kosa lake.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi