loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bora nianzie benchi - Messi

LIONEL Messi amesema hapendi kufanyiwa mabadiliko uwanjani bora aanzie benchi. Siku zilizopita, nahodha huyo wa Barcelona aligoma kufanyiwa mabadiliko wakati timu yake ikiwa inaongoza kwa idadi kubwa ya mabao.

“Sipendi kufanyiwa mabadiliko,” Messi aliiambia TyC Sports. “Napenda kuingia kutokea benchi kuliko nicheze kidogo kisha nitolewe.”

“Nasema hivyo kwa sababu mechi nyingi huamuliwa mwishoni mwa mchezo au unapata nafasi nyingi za kufunga kwa sababu wapinzani wakati mwingine huwa wamechoka, napenda kuingia kuliko nitolewe mapema.”

Messi amefunga mabao 674 katika michezo 829 aliyoichezea Barcelona na Argentina lakini alisema kufunga ni jambo moja katika mechi.

“Bado nadhani mimi sio mfungaji halisi,” alisema. “Napenda kuingia nyuma, kuwa na mawasiliano zaidi na mpira, kutengeneza nafasi.” “Pia napenda kuingia kwenye box, na kufunga.”

Messi pia alisema asingebadili mafanikio yake ya klabu kwa kushinda kombe la dunia 2014 Brazil. Ujerumani iliifunga Argentina bao 1-0 kwenye fainali hizo na Messi amweka wazi asingeweza kubadili maisha yake ya soka kushinda taji hilo.

“Ningependa nishinde taji la dunia na ilikuwa moja kati ya ndoto zangu kubwa, lakini nisingeweza kubadili chochote,” aliongeza.

MOHAMED Salah, alifunga mara mbili na kusaidia mabingwa Liverpool kufi ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi