loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Messi apiga mbili Barca ikishinda 5-1

NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi, alifunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili wakati timu yake ya Barcelona ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Real Valladolid na kurejea kileleni mwa msimamo wa La Liga.

Beki wa Barcelona, Clement Lenglet, alifunga bao la mapema, huku lile la kufutia machozi la Valladolid likifungwa na Olivas Alba katika dakika ya 15. Arturo Vidal alichukua mpira kutoka kwa Messi kabla hajaifungia Barcelona bao la kuongoza, kabla nyota huyo wa Argentina hajafunga kwa mkwaju wa adhabu likiwa ni bao lake la 50 la aina hiyo katika historia yake ya soka.

Messi alifunga la nne na baadae alimtengenezea, Luis Suarez, ambaye alifunga kitabu cha mabao kwa kufunga la tano. Barcelona haikushuka kiwanjani wikiendi baada ya mchezo wao wa El Classico dhidi ya Real Madrid kuahirishwa kutokana na hofu ya usalama inayoendelea huko Catalonia.

Hatua hiyo iliwafanya vibonde Granada, ambao wamerejea katika Ligi Kuu msimu huu kupata nafasi ya kushika uongozi wa La Liga wakati wakiwafunga Real Betis 1-0. Mapema juzi, Atletico Madrid walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Alaves.

MOHAMED Salah, alifunga mara mbili na kusaidia mabingwa Liverpool kufi ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi