loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hongera JWTZ kukamilisha ujenzi

TUNAWAPONGEZA wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kukamilisha agizo la Rais John Magufuli la kujenga nyumba za makazi ya askari Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Tunawapongza kwa sababu, kazi ya kijenga nyumba na kuzikamilisha kwa muda sio jambo dogo.

Tumeona wakandarasi wengi wakiingia mikataba ya ujenzi wa majengo makubwa na mwisho kuishia kubeba lawama za ama kuchelewesha kazi bila sababu za msingi, au kushindwa kumaliza kabisa.

Kazi hii ya ujenzi wa nyumba hizo ilikuwa imepelekwa kwa wabobezi wa ujenzi, yaani Wakala wa Majengo nchini (TBA) tangu mwaka 2016 kwa gharama ya Sh bilioni 10 na baada ya ujenzi huo kusuasua, ndipo Machi mwaka huu, Rais Magufuli akaamua kuwakabidhi JWTZ kukamilisha kazi hiyo.

Ikumbukwe, ni wanajeshi hao hao waliokamilisha kwa muda waliopewa na Rais Magufuli wa kujenga ukuta wa mirerani, jambo ambalo Watanzania wengi walidhani ni kazi ngumu isiyowezekana, lakini kwa uwezo mkubwa wakaweza kuikamilisha tena kwa ustadi mkubwa.

Hawa ndio wanajeshi wa Watanzania ambao hawashindwi wanapokuwa katika kutimiza majukumu yao ukiacha mbali ya majukumu mazito ya kulinda mipaka ya nchi, watu na rasilimali za taifa.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbuge, alisema jana kuwa jeshi limeshakamilisha ujenzi wa nyumba hizo tangu Oktoba 15 mwaka huu ambazo ni maghorofa 12.

Tunafuraha kwamba kukamilika kwa ujenzi wa maghorofa hayo kunatoa fursa kwa familia 172 za askari na maofisa magereza kuishi ndani yake.

Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Mbuge, wakati wowote atakwenda kuzikagua nyumba hizo na akijiridhisha atampa taarifa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo, ili naye azikague na kisha amwombe Rais Magufuli aweze kuzifungua rasmi.

Akasema japo alimwahidi Rais kuzikamilisha nyumba hizo katika kipindi kisichozidi miezi miwili na nusu tangu akabidhiwe Machi 16 mwaka huu, lakini kutokana na changamoto ya upatikanaji wa fedha haikuwezekana kukamilisha ujenzi ndani ya muda aliosema.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa JKT, kama nyumba hizo zingejengwa kama alivyotaka Rais Magufuli tangu mwanzo, zingeweza kuchukua familia 326.

Wakati alipotembelea ujenzi wa nyumba hizo Machi 16 mwaka huu, Rais Magufuli alichukizwa na kitendo cha TBA kushindwa kukamilisha ujenzi kwa zaidi ya miaka miwili tangu wakabidhiwe kazi hiyo mwaka 2016.

JWTZ wameshafanya mambo mengi ambayo ni vigumu kuyaorodhesha, kwani ni hao hao waliopewa kazi ya kusimamia hata zao la korosho kwa muda mfupi kama jinsi Rais Magufuli alivyoelekeza kwa kutumia nguvu na rasilimali zao, hivyo itoshe tu kusema kwamba tuna imani sana na jeshi hilo.

GEITA ni mmoja wa ...

foto
Mwandishi: Tahariri,

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi