loader
Picha

Magufuli- CAG usibishane na Bunge, Mahakama

Rais John Magufuli amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere atekeleze maagizo ya Bunge na Mahakama na asibishane nao.

Amempa agizo hilo Ikulu Dar es Salaam baada ya kumuapisha na pia kuwaapisha majaji na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Katarina Revokati.

Kabla ya uteuzi huo Katarina alikuwa Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania.

Amemtaka CAG asimamie miiko na mipaka yake ya kazi na asijifanye ni muhimili mwingine.

“Usije ukaenda huko ukajifanya na wewe ni muhimili, mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa kuna Mahakama, Bunge na sisi wa Serikali”amesema.

Kabla ya uteuzi huo, Kichere alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, na pia amewahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Na katika kiapo chako nilikuwa nakisikiliza, nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo, mwenye serikali yupo, kafanye kazi zako vizuri za ukaguzi bila kuonea watu.

Unapopewa maagizo na mihimili mingine kama Bunge katekeleze, usibishane nao. Ukipewa maagizo na mihimili kama Mahakama kaitekeleze, wewe ni mtumishi.”amesema Rais.

Rais Magufuli pia amewataka majaji aliowaapisha kusimamia miiko ya haki na usawa katika kutoa uamuzi wa kisheria kupitia na watoe haki na kwa wakati sahihi.

Amesema baadhi ya viongozi wamekuwa wakitishiwa nafasi zao kutokana na kusimamia haki, na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa majukumu yao.

Ametoa mfano wa mmoja wa majaji aliowaapisha kuwa alisimamishwa kazi katika Tume ya Ushindani (FCC) na alirudishwa baada ya kubainika kuwa tuhuma dhidi yake hazikuwa za kweli.

“Huyu akiwa anafanya kazi alishaamriwa kufukuzwa, ni kwa sababu tu alisimamia haki, na walikuwa wanamshangaa kumuona mchaga gani hapendi hela hela, wakacheza mbinu pale afukuzwe” amesema Rais Magufuli.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Ombeni Utembele

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi