loader
Picha

Sasa Tanzania tuna mashirika imara ya ndege, reli, bandari

WAKATI wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ukonga kuna klipu moja ilikuwa inarushwa na watu waliojitambulisha kama Chadema Hot News ikimkariri Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akisema: “Kama kuna kitu cha msingi kwa maisha ya Watanzania siyo ndege, siyo reli, siyo barabara… Mambo ya msingi ni uhuru na haki.”

Duh! Ndege, barabara, reli siyo vitu vya msingi katika nchi? Nilishangaa sana kusikia huyu mwenyekiti ambaye aliwahi kugombea urais wa nchi yetu akisema hayo, tena katika mkutano wa hadhara! Katika mwendelezo wa kulazimisha kukejeli kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano, chama hicho pia kimekuwa kikidai kwamba eti kipaumbele cha Watanzania ni chakula na maji na siyo ndege, barabara, reli wala umeme!

MASHIRIKA YA UMMA

Lakini wengi tungali tunakumbuka kwamba kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wapinzani wanaokejeli leo hatua muhimu na madhubuti zinazochukuliwa na serikali katika kuboresha mambo mbalimbali nchini, ndio hao hao waliokuwa wakiiponda serikali ya CCM kwa kuacha mashirika ya umma yakizorota. Walieleza, na siyo mara moja, jinsi wanavyosikitishwa na kuchungulia kaburi kwa mashirika kama ya reli (Shirika la Reli Tanzania -TRC), meli (sasa Wakala wa Meli Tanzania - TASAC), bandari (Mamlaka ya Bandari Tanzania –TPA), ndege (Shirika la Ndege Tanzania – ATCL), Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) na kadhalika. Walisema ni aibu kwa nchi ambayo imepata uhuru kwa zaidi miaka 50 kukosa shirika la ndege la kujivunia huku wakisema ilikuwa ni aibu watumishi wa umma wa Tanzania kupanda ndege za Kenya hata kwa safari za nchini.

Malalamiko haya yalikuwa ya kweli na siyo wapinzani tu walioona kasoro hiyo, bali Watanzania wengi wenye kuitakia mema nchi yetu. Hata mimi niliwahi kusafiri kwenda Uganda mwaka 2013 kuhudhuria vikao vya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje lakini niliondoka Dar hadi Nairobi kwa ndege za Shirika la Kenya (KQ) ambako niliunga ndege nyingine ya Kenya kwenda Entebbe, Uganda. Kurudi pia hali ilikuwa vivyo hivyo.

Kila nilipokuwa ninafika katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, roho ilikuwa ikiniuma sana namna nilivyokuwa ninaona ndege lukuki za KQ katika uwanja huo huku ukitua katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam unaweza kuona ‘kadege kamoja’ tu ka-ATCL au usione kabisa! Si bungeni pekee bali hata kwenye mikutano ya kisiasa aibu hii ilikuwa ikizungumzwa huku ikiunganishwa na jinsi nchi yetu inavyoonekana haina dhamira ya kweli ya kukuza utalii kulingamisha na majirani zetu ambao kwa kuwa na ndege za uhakika walikuwa ‘wanatupiga bao’.

Ukija kwenye reli ndio mengi sana yalisemwa. Kwamba ni nchi gani duniani inayotazamia kukuza uchumi wake huku ikaacha shirika la reli likilegalega wakati duniani kote reli ndio usafiri wa uhakika wa watu na mizigo? Na kwa kweli ilikuwa inashangaza kuona nchi kama Tanzania inayozungukwa na nchi nyingi ambazo hazina bandari kuliko nchi yoyote Afrika, ikiwaza kukuza bandari yake ya Dar es Salaam huku ikiwa haina reli ya uhakika!

Kwa kukosa reli ya uhakika ni wazi tulikuwa tunadhoofisha bandari ya Dar es Salaam na kusababisha gharama za usafirishaji kuwa kubwa, si kwa wafanyabiashara wa nje pekee bali hata wa ndani. Mfano wa hili unaweza ukaliona kwenye bei ya bidhaa mbalimbali ikiwemo saruji inayouzwa katika mikoa iliyo mbali na viwanda vinavyozalisha saruji.

Kuna wakati kabla serikali haijaingilia kati, saruji kutoka Uganda ilikuwa ikikimbiliwa na watu wengi katika mji wa Musoma kulinganisha na saruji ya Tanzania inayotoka katika mikoa ya Dar, Tanga au Mbeya na kusafirishwa kwa njia ya barabara. Hii ilikuwa ni kutokana na saruji za Tanzania (Simba, Tembo au Twiga) bei yake kuwa ghali kutokana na usafirishaji wake wa kutumia malori.

MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA

Lakini, kama wanavyosema Waswahili kwamba mwenye macho haambiwi tazama, tangu Rais John Magufuli aingie madarakani kila kitu kiko wazi. Tukianza na shirika la ndege, juzi tu Watanzania wamepokea ndege ya saba kati ya 11 zinazotarajiwa kununuliwa na serikali. Hatua hiyo imelifanya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuanza kuchanua.

Mbali na safari za ndani limeanza pia kupata safari za nje. Bila shaka sasa ni mwendawazimu tu anayeweza kusema serikali imeliacha shirika lake la ndege likichungulia kaburi! Kwa upande wa reli, licha ya reli ya sasa kuboreshwa na hadi kufufuliwa tena njia ya reli kati ya Tanga na Arusha, Tanzania inajenga reli ya kisasa ambayo ikikamilika, usafiri wa reli ndio itakuwa ‘habari ya mjini’.

Wengi wanakumbuka jinsi nchi yetu ilivyokuwa inasumbuliwa na umeme wa mgawo tena wakati huo Watanzania waliokuwa wakipata umeme wakiwa chini ya asilimia 20. Lakini wakati takwimu za sasa zinaonesha kuwa tumeshavuka asilimia 60 ya Watanzania wanaopata umeme ambao si wa mgawo kama ilivyoanza kuzoeleka, serikali ya Magufuli imepania kukata mzizi wa fitina kwa kuanza kujenga bwawa la umeme wa maji la Nyerere. Umeme utakaozalishwa ni mwingi kuliko umeme wote unaozalishwa kwa sasa hapa nchini.

NCHI BILA BARABARA, RELI, NDEGE

Mbowe alikaririwa akisema kwamba, ndege, reli, barabara siyo kitu muhimu kwa Watanzania hali inayoonesha kwamba pengine hajui faida za uboreshaji wa miundombinu ya usafiri inayochukuliwa kama damu kwenye mwili wa mwanadamu. Kwanza, usafiri unapoboreka unapaisha utalii wa ndani na kuongeza mapato ya wananchi na taifa.

Kwa wakulima, usafiri unapokuwa rahisi unaogeza bei ya mazao ya kilimo na bei ya mifugo na pia unapunguza muda na gharama za usafirishaji. Usafiri unaboresha undugu baina ya eneo moja ambalo lilikuwa halifikiki kirahisi na lingine na pia unasaidia watu ambao wanapitiwa na usafiri wao na vitu vyao kuonekana (exposure) na kupata huduma nzuri zaidi. Usafiri unaboresha biashara baina ya eneo moja na lingine

MAFUNZO ya uongozi na usimamizi wa elimu ni ...

foto
Mwandishi: Hamisi Kibari

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi