loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mbape anukia Real Madrid

MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe atacheza Real Madrid siku zijazo, kwa mujibu wa makamu wa rais wa zamani wa Monaco, Vadim Vasilyev.

Mrusi huyo alikuwa Monaco Mbappe akiaza harakati zake za soka na pia ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuhamia PSG kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20.

Vasilyev alisema, licha ya kutakiwa na baadhi ya klabu kubwa Ulaya, Mbappe aliamua kubaki nyumbani kwa lengo la kukua zaidi.

“Kylian aliniambia: ‘Vadim, naisikia hii ndani kabisa ya moyo wangu, ni mapema mno [Kuondoka Ufaransa],’” kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 54 aliiambia Telefoot.

“’Nimechezea nchi yangu mara moja tu.”

“’Sitaki kuiacha nchi yangu hivi, nataka kuwa mchezaji mkubwa hapa, Real inaweza kusubiri.”

Vasilyev aliongeza kuwa hana shaka yoyote kwamba Mbappe atamalizia soka yake Real Madrid.

“Nilimwambia watafurika uwanja wa Santiago Bernabeu wakikupigia makofi utakapowasili, uhitaji uthibitisho kulijua hilo.”

Vasilyev na Mbappe walipata chakula cha mchana pamoja baada ya PSG kuifunga Marseille mabao 4-0 kwenye Ligue 1.

“Ni Kylian yuleyule, mshindani yuleyule mtu yuleyule aliyetaka kushinda kila kitu, kila kitu na kila kitu haijalishi gharama,” aliongeza.

MOHAMED Salah, alifunga mara mbili na kusaidia mabingwa Liverpool kufi ...

foto
Mwandishi: PARIS, Ufaransa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi