loader
Picha

Mafanikio ya NSSF na miaka minne ya kishindo cha Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linampongeza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika uongozi wake kwa kipindi cha miaka minne tangu aingie madarakani Novemba 2015.

Pamoja na mambo mengi makubwa ya maendeleo aliyoyafanya kwa Taifa letu la Tanzania ambayo ni pamoja na ununuzi wa ndege kumi na moja (11) na kulifufua Shirika la ndege la Tanzania, Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge), ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme katika bonde la mto Rufiji (Stigglers Gorge), ujenzi wa barabara nyingi nchini zinazounganisha maeneo yote ya nchi, Ujenzi wa Hospitali, vituo vya afya, Shule za msingi na Sekondari, uboreshaji wa huduma za afya kwa kuongeza bajeti ya madawa na vifaa tiba, pia ameboresha sekta ya Hifadhi ya jamii nchini.

Uboreshaji wa sekta ya Hifadhi ya jamii nchini umeenda sambamba na marekebisho ya sheria ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF) kwenye sura ya 50 ya mwaka 2018 ambapo sasa NSSF inatoa huduma ya Hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi walio katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bwana William Erio amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya NSSF, Shirika linatekeleza majukumu makuu manne ambayo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.

Katika kutekeleza majukumu ya Shirika, Bwana Erio amesema kuwa Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuboresha maisha ya Watanzania hivyo kupitia mabadiliko ya sheria ya Hifadhi ya jamii sura ya 50 ya mwaka 2018, NSSF imeweza kuwafikia na kuwaandikisha wanachama kutoka sekta binafsi. Kwa mujibu wa sheria waajiri wote nchini kutoka sekta binafsi wanatakiwa kuandikisha wafanyakazi wao kwenye shirika la NSSF.

Katika kipindi cha miaka minne Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli ameweza kuwasaidia wananchi waliojiajiri wenyewe ambao wengi wao ni Wakulima, na wajasiriamali; Kwanza kwa kuwapunguzia mzigo wa kodi na ushuru, Pili amewawezesha wajasiriamali kufanya biashara zao bila kubugudhiwa na kuwakabidhi vitambulisho ikiwa ni utambulisho wa kufanya biashara sehemu yeyote ambapo mkakati huo unawajengea uwezo wakupata faida kwenye biashara zao na kuwawezesha kujiandikisha na NSSF ili kujiwekea akiba kwa ajili ya uzee, ulemavu, vifo, maradhi na majanga mengine ambayo yatasababisha kundi hili la Watanzania kushindwa kufanya shughuli zao na hatimaye kukosa kipato cha kuendesha maisha yao na familia zao.

Jukumu la pili la NSSF ni kukusanya michango, NSSF imeweza kuboresha njia ya ukusanyaji michango kutoka kwenye utaratibu wa kupokea hundi na pesa taslimu hadi kujiunga na mfumo wa malipo wa Serikali Kieletroniki (GePG); Mfumo huu umeleta tija kwenye ukusanyaji michango ya wanachama.

Katika kipindi cha mwaka mmoja 2018/19 kiasi cha shilingi 828.1 bilioni ilikusanywa. Mfumo wa GePG umeendelea kuwa na matokeo chanya kwa NSSF. Awali makusanyo yalikuwa Shilingi 60 bilioni kwa mwezi kwa sasa makusanyo ya michango yameongezeka na kufikia kiasi cha shilingi 96.1 bilioni kwa mwezi. Mkurugenzi Mkuu huyo ameendelea kusema kuwa NSSF inaendelea kuboresha uwekezaji ambapo sasa Shirika linawekeza zaidi kwenye dhamana za Serikali.

"Tumeweza kuongeza kiasi cha kuwekeza kwenye dhamana za Serikali kutoka asilimia 8 iliyokuwepo mwezi Agosti 2018 hadi kufikia asilimia 20 tarehe 30 Juni 2019. Hivyo basi hadi kufikia Agosti 2019, NSSF iliwekeza jumla shilingi 733.8 bilioni kutoka shilingi 340.5 bilioni zilizokuwa zimewekezwa mwezi Juni 2018”.

Katika kipindi cha mwaka mmoja ulioishia mwezi Juni 2019, Shirika liliendelea kuhakikisha kuwa linaboresha mapato yatokanayo na uwekezaji. Mfano mmoja ni eneo moja la mradi wa daraja la Mwalimu Nyerere, Kigamboni ambako makusanyo yake yameongezeka toka wastani wa shilingi 697.4 Milioni kwa mwezi Agosti 2018 hadi kufikia shilingi 1.08 bilioni kwa mwezi mmoja wa Julai 2019 hili ni ongezeko la zaidi ya asilimia 54 katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda, NSSF imeendelea kuwekeza katika viwanda mbalimbali kama vile kukiwezesha kiwanda cha viua wadudu Kibaha kwa kuwakopesha mtaji, pia Shirika limetoa mkopo kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ili waweze kufufua kiwanda cha unga wa Mahindi na kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti kilichopo jijini Dodoma. Shirika limeendelea na ulimaji wa mashamba ya miwa na hatua za awali za ujenzi wa kiwanda cha sukari katika eneo la Mbigiri mkoani Morogoro zinaendelea.

Hii yote ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kupitia ujenzi wa viwanda. Katika kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais za kuwaletea maendeleo Watanzania na kutatua kero zao nyingi kwa kuboresha mifumo yao ya malipo na hasa kuwawezesha wastaafu kupokea mafao yao moja kwa moja kupitia akaunti zao za benki badala ya kwenda kupanga misululu katika ofisi za NSSF.

Uboreshaji wa mifumo umesaidia kupunguza malalamiko kwa wanachama wao kwenye ucheleweshaji wa malipo yao baada ya kuanza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika ulipaji wa mafao ambayo kwa ujumla wake imerahisisha malipo ya wanachama.

MAFUNZO ya uongozi na usimamizi wa elimu ni ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

1 Comments

  • avatar
    Said Tandika
    05/11/2019

    Bravo, it is good advance in making sure we get bews at our finger tips!

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi