loader
Picha

Kikao kizito kinaendelea Yanga, Zahera ndani

HUKU taarifa zikivuma kwenye mitandao ya kijamii kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefutwa kazi, kikao kizito kinaendelea muda huukwenye ofisi za Klabu hiyo zilizopo Jangwani, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Zahera akiwa amevaa ‘bukta’ akitokea kusimamia mazoezi ya klabu hiyo aliingia kwenye kikao hicho na hadi sasa hakuna taarifa zilizowekwa bayana kuhusu kutimuliwa kwa kocha huyo mwenye majigambo.

Taarifa zilizotolewa kwenye mitandao zinaeleza kuwa aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Bernard Mwalala ndiye alitakayechukua mikoba ya Zahera.

Waandishi wa habari wamekusanyika makao makuu ya klabu hiyo kupata ufafanuzi wa taarifa hiyo.

Mwishoni mwa juma, Yanga ilitolewa kwenye michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa kipigo cha jumla ya mabao 4-1 kutoka kwa Pyramids ya Misri.

Siku za hivi karibuni, mashabiki wamembadilikia kocha huyo wakidai kuwa timu haichezi vizuri huku wakishinikiza Mkongo huyo aondolewe.

BOSTON Marathon sasa imefutwa kabisa ikiwa ni mara ya kwanza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi