loader
Picha

Tanzanite yaiingizia Serikali bil 1.8/-

KUANZIA Januari hadi Oktoba mwaka huu, madini ya Tanzanite ya Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara yameiingizia serikali Sh bil 1.8, baada ya tathimini ya ukuta uliojengwa.

Ofisa Madini Mfawidhi Kanda ya Mirerani, Daud Ntalima alisema hayo jana alipozungumza na wachimbaji wadogo maarufu kwa jina la wana Apollo, mama lishe, wanunuzi wadogo na viongozi wa vijiji vya Naisinyai na Mirerani katika ofisi ya Wizara ya Madini Mirerani.

Ntalima alisema kiasi hicho kilichokusanywa mwaka huu kilitokana na makusanyo ya kilo 1,900 za madini hayo yaliyofanyiwa tathmini ndani ya ukuta na kiasi hicho kuingia serikalini.

Alisema, ongezeko hilo kwa mwaka huu ni zaidi ya mara mbili ya madini ya mwaka jana, kwani mwaka 2018, serikali iliingiza Sh bil 1.4 baada ya madini kilo 781 kufanyiwa tathimini ndani ya ukuta na kulipiwa kodi halali ya serikali.

Ofisa huyo alisema madini kilo 1,900 yaliyopo nje ya ukuta ndio yaliyofanyiwa tathimni ndani ya ukuta na kuruhusiwa kutoka nje , lakini bado hayajafika katika masoko maalumu ya kuuza madini na wala hakuna nyaraka zinazoonesha yamesafirishwa nje ya nchi.

Alisema kuna makundi manane ya wamiliki wa migodi 325,wenye leseni za migodi 840,wana Apollo 8,700, wadhamini wa migodi 193, wanunuzi wadogo 450, wachuuzi wa magonga 4,455,mama lishe 560, raia wa nje ya nchi 130.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Mirerani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi