loader
Picha

Kila mchezaji muhimu-Aussems

KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema kila mchezaji ana umuhimu wa kucheza kwenye kikosi chake kwa vile wote anawahitaji katika kutetea taji la Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea katika mchezo wa Prisons utakaochezwa kesho, Aussems alisema kutokana na umuhimu wa kila mchezaji amekuwa akipanga kwa mzunguko ili kila mmoja apate nafasi ya kucheza.

“Tumekuwa tukifanya mzunguko wa kikosi chetu kumpa nafasi kila mmoja kwasababu ukichezesha kile kile kuna wengine wanaweza kukata tamaa,”alisema.

Alisema wachezaji wote wanahitajika hadi mwishoni mwa msimu kuhakikisha wanapambana kwa lengo la kutetea ubingwa. Kuhusu mchezo wa kesho dhidi ya Prisons alisema huenda ukawa mgumu kwa vile watakutana na timu ambayo haijapoteza mchezo wowote kutokana na ubora.

Alisema wachezaji wake wanaendelea vizuri kwa maandalizi ya mchezo huo ila wanakabiliwa na majeruhi wachache akiwemo John Bocco aliyeko nje kwa muda mrefu na wengine wanaendelea kutizamwa Miraji Athumani na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Wekundu hao wa Msimbazi wanaongoza ligi wakiwa na pointi 21 baada ya kucheza michezo minane, kushinda saba na kupoteza mmoja. Kwa upande wa Prisons wanashika nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 10, wakishinda minne na kupata sare sita.

NAHOD HA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi