loader
Picha

‘Bidhaa za Sanaa, Utamaduni huvutia watalii’

MWENYEKITI wa Tamasha la Urithi kitaifa, Profesa Martin Mhando amesema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuvutia watalii wengi zaidi kwa kutumia bidhaa za sanaa na utamaduni kwa kuangazia vionjo vya kipekee vinavyopatikana hapa nchini.

Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni wakati wa mahojiano na gazeti hili kuhusu tamasha la Urithi la Mtanzania mjini Mwanza huku pia, akitolea mfano namna tamasha la urithi la Dodoma lilivyoungana na lile la mvinyo na kufanikiwa kuwavutia watalii.

“Tamasha hili linaweza kuwa mahsusi hapa duniani tukitilia maanani utofauti wa mvinyo unaopatikana Dodoma uzuri wake na hata ukulima linaweza kufanya wapenzi wa mvinyo duniani wakamiminika mkoani humo kuona mizabibu, kuonja mvivyo na kuona utamaduni wa jamii zinazoizunguka” alisema.

Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alizungumzia umuhimu wa kutunza utamaduni uliopo na kujitambua.

“Kwa kujitambua sisi tunaweza kuwa na uthubutu na ubunifu mkubwa vitu ambavyo vinategema sana kujiamini” alisema.

Pia, aliusifu Mkoa wa Mwanza kuwa ni kitovu cha nchi zinazolizunguka Ziwa Victoria na hata kitamaduni hufanana na nchi za Uganda, Kenya, Burundi na Rwanda na hata Kongo.

“Kwa kutanguliza utamaduni ndio tumeona jinsi wanamwanza walivyoonesha umahiri wao katika mashindano ya kuendesha mitumbwi na hata baisikeli,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema alisikia furaha kuona kilele cha tamasha hilo likifanyika jijini kwake kwa sababu wana vivutio vingi ambavyo vingeweza kuvutia watalii kutoka Jumuia ya Afrka mashariki na hata kutoka nje.

“Machifu wetu ndio walinzi wakubwa wa urithi wa jadi zetu. Kazi tunayotaka kufanya Mwanza itajumuisha kuibua vipaji, na kupitia tamasha la Urithi tumeona dhahiri nafasi ya sanaa na utamaduni katika kutangaza utalii,” alisema.

Akifunga tamasha hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Khamis Kigwangalla alitilia mkazo umuhimu wa kuwa na matamasha ya aina hiyo ili kuinua wigo wa utalii nchini.

NAHOD HA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mwanza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi