loader
Picha

Kikosi cha Stars kitakachoivaa Equatorial Guinea chatajwa

KOCHA wa Taifa Stars, Etienne Ndairagije ametangaza kikosi cha wachezaji 27 kitakachoivaa Equatorial Guinea katika mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Afcon 2021.

Katika kikosi hicho, wachezaji saba wanatoka Simba huku wengine wakitoka katika vilabu vingine vinavyoshiriki Ligi Kuu Bara pamoja na mataifa mengine ndani na nje ya bara la Afrika.

Taifa Stars imepangwa Kundi J linalozijumuisha timu za mataifa ya Tunisia, Libya na Equatorial Guinea.

Orodha ya wachezaji hao inawajumuisha Juma Kasema (KMC), Metacha Mnata (Yanga), David Kisu (Gor Mahia), Salum Kimenya (TZ Prisons), Ramadhan Kessy (Nkana FC), Mohamed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Simba).

Wengine ni Erasto Nyoni (Simba), Bakari Kondo (Coastal Union), Kelvin Yondani (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Abdul-Aziz Makame (Yanga), Dickson Job (Mtibwa), Simon Msuva (Difaa El Jadid), Eliuter Mpepo (Buildcon), Iddi Suleiman (Azam FC), Salum Abubakar (Azam) na Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania).

Aidha kocha huyo amewajumuisha kikosini Shaban Iddi (Azam), Mzamiru  Yassin (Simba), Frank Domayo (Azam), Mbwana Samatta (Genk), Farid Mussa (Tenerrife), Miraji Athuman (Simba), Hassan Dilunga (Simba), Kelvin John (Football House) na Ayoub Lyanga (Coastal Union).

MAKUNDI YOTE KUFUZU AFCON 2021 CAMEROON

Kundi A: Mali, Guinea, Namibia, Liberia/Chad
Kundi B: Burkina Faso, Uganda, Malawi, Sudan Kusini/Shelisheli
Kundi C: Ghana, Afrika Kusini, Sudan, Mauritius/Sao Tome
Kundi D: DRC, Gabon, Angola, Djibouti v Gambia
Kundi E: Morocco, Mauritania, CAR, Burundi
Kundi F: Cameroon, Cape Verde, Msumbiji, Rwanda
Kundi G: Misri, Kenya, Togo, Comoro
Kundi H: Algeria, Zambia, Zimbabwe, Botswana
Kundi I: Senegal, Congo, Guinea Bissau, Eswatini
Kundi J: Tunisia, Libya, Tanzania, Equatorial Guinea
Kundi K: Ivory Coast, Niger, Madagascar, Ethiopia
Kundi L: Nigeria, Benin, Sierra Leone, Lesotho

TANZANIA imeitaka Dunia na Jumuiya za Kimataifa kutambua kuwa kauli ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    bushu masunga kutoka bariadi ya simiyu
    15/11/2019

    Comment

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi