loader
Picha

Wanunuzi wakubwa wa dhahabu mbaroni

SERIKALI imekamata wanunuzi tisa wakubwa wa dhahabu waliokuwa wakinunua madini hayo nje ya masoko.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema jijini Dodoma kuwa, tangu kuanzishwa kwa masoko hayo Machi mwaka huu yameongeza mapato hasa katika mauzo ya dhahabu.

Amesema serikali imeua mtandao wa ununuzi wa madini nje ya masoko hayo na sasa wauzaji na wanunuzi wananufaika.

Nyongo amesema hadi sasa kuna masoko zaidi ya 28 ya madini na yana matokeo chanya ya moja kwa moja.

Amesema, soko la madini mkoani Geita limeiwezesha Serikali kukusanya zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwezi kutoka shilingi milioni 440/- hadi shilingi milioni 500/- za awali.

“Ukienda Chunya dhahabu iliyokuwa inakusanywa kwa mwezi ni kilo 20 tu lakini sasa hivi tunavyozungumza kwa mwezi mmoja tunakusanya kilo zaidi ya 150, haya ni mabadiliko makubwa” amesema Nyongo wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Tisa la Uziduaji.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Serikali ilianzisha masoko ya dhahabu baada ya kujiuliza mchimbaji anapopata dhahabu anapeleka wapi na mnunuzi anayetaka kununua dhahabu anakwenda kununnua wapi.

“Mnunuzi na muuzaji hawakuwa na maeneo ya kukutana, tukasema ni lazima wanunuzi na wauzaji wa dhahabu tuwatengenezee mahala maalumu wakutane ili kusudi wauziane na wakiuziana Serikali Serikali iweze kuchukua tozo yake pale, ichukue mrabaha, ichukue clearance fee, halmashaur ichukue service levy yake kama kodi ya halmashauri na kwa kweli machimbaji wamefurahia masoko haya”amesema Nyongo.

MSEMO wa wahenga ‘Majuto ni mjukuu, huja baada ya kitendo’ ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo na Janeth Mesomapya

1 Comments

  • avatar
    MWL HAMZA SALUM
    07/11/2019

    HONGERA SANA DC WETU JWA KUELIMISHA WASIPENDA MAZURI ANAYOTUFANYIA RAIS WETU MPENDWA DR JOHN POMBE MAGUFURI, KIUKWELI WANAOMPINGA NI WALE WANAOYAONA MAZURI NA WANAYAFURAHIA LKN USHABIKI WA KIPUUZI WA KIVYAMA WANAMBEZA LKB WAKIENDA HSPTL WANAPATA HUDUMA VZR,ELIMU WANAPATA BURE,UMEME MGAO HAWAUJUI TENA,USALAMA WA KUTOSHA,BARABARA ZINAZIDI KUJENGWA,MAJI BOMBA MPAKA KIJIJINI,NAAPA KUTOKA MOYONI MUNGU KAIKUMBUKA TANZANIA NA NDIYO MAANA KAMSIMIKA MAGUFURI WATANZANIA TUCHEKE TUFURAHI NA TUJIVUNIE KUWA WATANZANIA,ASANTE MUNGU KUTUSIMIKIA JEMBE MAGUFURI,MPE AMANI,AFYA NJEMA NA UMRINDE AZIDI KUCHAPA KAZI, DC WETU PIA HATA WEWE UNACHAPA KAZI KULIKO KAWAIDA SIFICHI UKIAMUA JAMBO LAZIMA LIKAMILIKE HONGERA SANA NA MU GU AKUBALIKI

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi