loader
Picha

Zahera ataja Dk Msolla, Ndama wachawi wake

ALIYEKUWA Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amewataja watu waliosababisha ‘kitumbua’ chake kumwagiwa mchanga katika klabu hiyo.

Uongozi wa klabu ya Yanga juzi ulimtupia virago Zahera baada ya timu hiyo kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Pyramids ya Misri.

Katika mchezo wa kwanza, Yanga ilifungwa 2-1 Dar es Salaam. Akihojiwa na EFM jana, Zahera alimtaja mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Ndama aliyewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Mashindano na Usajili kuwa alihusika na kuondolewa katika timu hiyo.

Alisema Ndama wakati timu hiyo ikiwa nchini Misri kujiandaa na mchezo dhidi ya Pyramids alimpigia simu mwenyekiti wa timu hiyo Dk Mshindo Msolla akimtaka amtimue kocha huyo kwa kuwa haina matokeo mazuri.

“Msolla alinipigia simu wakati nikiwa Misri akisema kuwa kuna mtu (Ndama) anataka nikutimue kwa sababu timu imekosa ushindi, lakini Msolla alijibu kuona hakuona sababu za kunitimua kwa kuwa timu ilikuwa ikifanya vizuri, “alisema Zahera.

Aidha Zahera amemtaja Msolla kuwa naye alichangia kutimuliwa kwake baada ya kukataa kuchaguliwa kocha msaidizi wa kufanya kazi zake badala ya yule wa sasa Noel Mwandila.

Alidai kuwa Msolla alikuwa akimtaka Mkwasa kuwa msaidizi wa Zahera, lakini kocha huyo raia Congo hakuwa tayari kuchaguliwa msaidizi.

“Nikiwa Misri Msolla alinipigia simu kunihakikishia kutonifukuza kazi licha ya kupoteza mchezo, lakini alinambia msaidizi wangu Noel Mwandila mkataba wake unaisha mwishoni mwa mwaka huu na nikiwa na timu ya taifa (Congo), Yanga inafanya vibaya chini ya Mwandila. Kutokana na hivyo nataka tukuletee kocha mwingine msaidizi (Charles Mkwasa) mimi nilikataa na kumuambia siwezi kukubali hilo mbona naona anafanya majukumu yake vizuri kama vipi nisubiri nikisharudi tutaongea.”

Alisema kuwa aliporejea jijini Dar es Salaam kutoka Misri alikutana na makamu mwenyekiti Fredrick Mwakalebela na viongozi wengine wa benchi la ufundi na kufanya kikao cha dharura, lakini aliwaeleza kuwa hawezi kuchaguliwa msaidizi na ataendelea kufanyakazi na Mwandila. Alipotafutwa jana kwa njia ya simu, Mkwasa alisema kuwa wakati huo alikuwa safarini kwenda Mtwara kucheza na Ndanda, wakati Msolla na Ndama simu zao hazikupatikana.

NAHOD HA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi