loader
Picha

Simba, Prisons ubabe leo

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Simba leo wanashuka dimbani kuwakabili Tanzania Prisons katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru. Unaweza kuwa mchezo wa kibabe kutokana na wapinzani wao Prisons kuwa timu ya pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu msimu huu.

Simba ikiwa ni kinara inaongoza kwa pointi 21 baada ya kucheza michezo minane, kushinda saba na kupoteza mmoja. Kabla ya michezo ya jana ya Ligi kwa timu nyingine, Prisons ilikuwa inashika nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 10, kushinda minne na sare sita huku ikiwa na pointi 18.

Iwapo wekundu hao wa Msimbazi watashinda leo basi wataendelea kujikita kileleni na kuwaacha wengine mbali lakini kama watapata sare bado pia watakuwa juu na wakipoteza na Prisons wakashinda basi watalingana kwa pointi sawa 21.

Simba ni timu yenye safu bora ya ulinzi kwani katika michezo minane imeruhusu mabao matatu pekee katika nyavu zake, ikiongoza kwa safu bora ya ushambuliaji kwa kufunga jumla ya mabao 16 huku Meddie Kagere na Miraji Athumani wakiongoza kutupia katika timu hiyo mmoja akifunga manane na mwingine manne.

Timu ya maafande hao wa Mbeya imekuwa ikicheza kwa kujihami zaidi na mashambulizi ya kushtukiza kwasababu wanaongoza kwa sare nyingi yaani sita na hata safu ya ushambuliaji inajitahidi kwa kiasi kutokana na kufunga mabao 13 pekee na kuruhusu kufungwa mabao manane.

Kocha wa Simba Patrick Aussems alisema anategemea mchezo huo utakuwa ni mgumu akiamini wapinzani wake ni bora kutokana hawajapoteza mchezo wowote. Kocha wa Prisons, Adolf Rishard alisema anawaheshimu Simba ni timu kubwa wataingia uwanjani kwa tahadhari kwa lengo la kupambana na kupata matokeo mazuri.

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi